Giacomo Benefatti
Mandhari
Giacomo Benefatti (alifariki 19 Novemba 1332) alikuwa padre wa Kanisa Katoliki wa Italia na mtawa wa shirika la Wahubiri (Order of Preachers), ambaye alifikia cheo cha Askofu wa Mantova. Benefatti alijulikana kwa huduma yake ya upole kwa wagonjwa hasa wakati wa milipuko ya tauni, na Papa Benedikto XI - ambaye alikuwa rafiki wake wa karibu - na Papa Yohane XXII walimheshimu sana.[1]
Sifa ya Benefatti ya utakatifu binafsi iliendelea kuwa maarufu kwa karne kadhaa baada ya kifo chake, na kuthibitishwa na Papa Pius IX kwa kumtangaza askofu huyo kuwa mwenye heri mnamo 22 Septemba 1859.[2]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Blessed James Benefatti". Saints SQPN. 26 Novemba 2015. Iliwekwa mnamo 10 Agosti 2016.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Blessed Giacomo Benefatti of Mantua". Santi e Beati. Iliwekwa mnamo 10 Agosti 2016.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
| Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |