Nenda kwa yaliyomo

Ghuba ya Menai

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mandhari ya Ghuba ya Menai kwa picha ya satelaiti

Ghuba ya Menai ni ghuba iliyopo katika Wilaya ya Mkinga ya Mkoa wa Mjini Magharibi, Tanzania. Kijiografia, ghuba hii ni sehemu ya Visiwa vya Zanzibar.

Jiografia

[hariri | hariri chanzo]

Ni ghuba yenye upana wa takribani kilomita 10 katika Mfereji wa Zanzibar wa Bahari ya Hindi ya Magharibi.[1] Ukanda mrefu wa pwani ya Ghuba ya Menai una vijiji kumi na tisa vyenye jumla ya wakazi wapatao 17,000. Vijiji hivi viko ndani ya Mkoa wa Kusini Unguja wa Zanzibar. Eneo la Hifadhi ya Ghuba ya Menai (MBCA) ni hifadhi ya bahari inayolinda makazi na viumbe wa ghuba hiyo.[2]

Uharibifu wa mikoko

[hariri | hariri chanzo]

Mikoko katika Ghuba ya Menai iliyo karibu na makazi kama Unguja Ukuu, Pete, na Uzi imeathirika zaidi. Hivyo basi, sehemu ya magharibi ya Menai ina uharibifu mkubwa zaidi wa mikoko kuliko upande wa mashariki. Ingawa kuna sheria na kanuni zilizopo kwa ajili ya kupunguza uharibifu huo, kasi ya kupungua kwa mikoko Zanzibar ni ya kutia wasiwasi. Spishi za mikoko zilizoathiriwa zaidi ni B. gymnorrhiza, R. mucronata, na C. tagal.[3]

Kuna spishi nane za pomboo katika maeneo ya karibu na Zanzibar; hata hivyo, ni mbili tu zinazoishi kwa mwaka mzima katika Eneo la Hifadhi ya Ghuba ya Menai (MBCA), ambalo liko nje ya pwani ya kusini-magharibi ya Kisiwa cha Unguja. Spishi hizi ni Indo-Pacific bottlenose dolphin (Tursiops aduncus) na Indian Ocean humpback dolphin (Sousa plumbea). Spishi hizi mbili ziko hatarini kutokana na utalii unaotumia boti na pia kukamatwa kwa bahati mbaya wakati wa uvuvi. Hatari yao inaonekana katika makadirio madogo ya idadi: S. plumbea - 35, na T. aduncus - 136. Hadi sasa hakuna usimamizi maalum uliowekwa kwa ajili ya ulinzi wa spishi hizi dhidi ya uvuvi au utalii. Aidha, hakuna utafiti uliowahi kufanyika hapo awali kuhusu tofauti katika usambazaji, uwepo au tabia zao. Taarifa kuhusu athari za kimazingira na shughuli za binadamu kwa usambazaji wa spishi hizi pia ni chache.[4]

  1. Google Earth
  2. WWF: taarifa kuhusu Eneo la Hifadhi ya Ghuba ya Menai
  3. Mohamed, Mohamed Khalfan, Elhadi Adam, na Colbert M. Jackson. "The spatial and temporal distribution of mangrove forest cover from 1973 to 2020 in Chwaka Bay and Menai Bay, Zanzibar." Applied Sciences 13.13 (2023): 7962.
  4. Temple, Andrew J., et al. "Spatial and temporal variations in the occurrence and foraging activity of coastal dolphins in Menai Bay, Zanzibar, Tanzania." PloS one 11.3 (2016): e0148995.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]