Nenda kwa yaliyomo

Ghuba ya Lindi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ghuba ya Lindi

Ghuba ya Lindi ni eneo la maji lililopo kusini mwa Mkoa wa Lindi katika mashariki ya kusini mwa Tanzania. Iko katika Bahari ya Hindi, ghuba hii ina urefu wa kilomita 11.8, upana wa kilomita 5.9 katika sehemu pana zaidi, na mita 750 katika sehemu nyembamba zaidi. Ghuba inalishwa na Mto Lukuledi, ambapo mdomo wa mto huo kuingia ghuba uko katika mji wa Lindi, ambao pia ni makao makuu ya mkoa wa Lindi. Ghuba haina bandari yenye uwezo wa kupokea meli, hata hivyo, vyombo vya usafiri wa majini vinavyotumika zaidi ni kivuko cha Lindi pamoja na mitumbwi inayotumiwa na wavuvi waishio eneo hilo.[1] Wakazi wa asili wa ghuba hii ni Wamwera.

  1. "Lindi Bay bay, Lindi, Tanzania". tz.geoview.info. Iliwekwa mnamo 2021-07-22.
Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Lindi bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Ghuba ya Lindi kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.