Gholam Hossein Sadighi
Gholam-Hossein Sadighi (3 Desemba 1905 – 28 Aprili 1991) alikuwa mwanasiasa wa Iran na Waziri wa Mambo ya Ndani katika serikali ya Waziri Mkuu Mohammad Mosaddegh mnamo mwaka 1953. Baada ya mapinduzi ya kijeshi yaliyofadhiliwa na CIA kumgong'oa Mossadegh, Sadighi alikamatwa na baadaye alitoa ushahidi wa kumtetea Mossadegh wakati wa kesi yake. Licha ya kupoteza madaraka, Sadighi aliendelea kuwa hai kisiasa. Alisaidia kuunda chama cha "Second National Front" mnamo mwaka 1960 na, pamoja na wanasiasa wengine waliomuunga mkono Mossadegh, alipigania mfumo wa kidemokrasia na Shah ambaye anatawala lakini haongozi serikali.
Kufikia mwaka 1978, Iran ilikuwa imekumbwa na machafuko makubwa na kulikuwa na hatari kubwa kwamba Mohammad Reza Pahlavi angepinduliwa na uasi wa umma ulioongozwa na Ayatollah Ruhollah Khomeini. Kutokana na tishio hili, Shah alijaribu kumteua Sadighi kuwa waziri mkuu ili kuwakusanya wanasiasa wenye msimamo wa wastani kuunga mkono serikali na kudhoofisha upinzani wa kidini.[1] Hata hivyo, mpango huo ulishindikana kutokana na Sadighi kusisitiza kuwa Shah lazima abaki nchini humo na kwamba mamlaka kamili ya uendeshaji yawekwe mikononi mwa baraza la mawaziri la waziri mkuu, mambo mawili ambayo Shah alikataa kuyakubali. Kwa sababu hiyo, Sadighi alijiondoa na badaye Shah akamteua Shapour Bakhtiar (mmoja wa viongozi wengine wa National Front) kuwa Waziri Mkuu. Sadighi alikuwa mzalendo ambaye hakuwahi kuondoka Iran na aliishi Tehran hadi kifo chake mnamo Aprili 1991. Alizikwa katika Makaburi ya Ibn Babawayh huko Ray.
Maisha ya binafsi
[hariri | hariri chanzo]Sadighi alimuoa Farahangiz Meftah na walibarikiwa kupata binti wawili (Afarin na Nikou Sadighi) na mtoto mmoja wa kiume (Hossein Sadighi).
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Darioush Bayandor (2019). The Shah, the Islamic Revolution and the United States. Cham, Switzerland: Palgrave Macmillan. uk. 283. doi:10.1007/978-3-319-96119-4. ISBN 978-3-319-96118-7. S2CID 158585193.
| Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Gholam Hossein Sadighi kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |