Gervais Banshimiyubusa
Mandhari
Gervais Banshimiyubusa (alizaliwa 9 Septemba 1952) ni kiongozi wa Kanisa Katoliki kutoka Burundi ambaye anahudumu kama Askofu mkuu wa Jimbo Kuu la Bujumbura, Burundi, tangu mwaka 2018. Kabla ya hapo, kuanzia Desemba 2002 hadi Machi 2018, alikuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Ngozi, Burundi.
Kabla ya hapo tena, alihudumu kama Askofu Msaidizi wa Jimbo la Ngozi kuanzia Mei 2000 hadi Desemba 2002.[1] Pia alihudumu kama Msimamizi wa Kikanisa wa jimbo la Ngozi kuanzia tarehe 24 Machi 2018 hadi 25 Januari 2020. Aliteuliwa kuwa Askofu tarehe 10 Mei 2000 na Papa John Paul II.[2][3]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Davis M. Cheney (19 Julai 2024). "MicroData Summary for Archbishop Gervais Banshimiyubusa (born 9 September 1952), Archbishop of Bujumbura". Kansas City. Iliwekwa mnamo 19 Februari 2025.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Agenzia Fides (26 Machi 2018). "Africa/Burundi: Resignation of the Archbishop of Bujumbura and appointment of the new Archbishop". Agenzia Fides. Vatican City. Iliwekwa mnamo 19 Februari 2025.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Gilbert Nsavyimana (29 Juni 2018). "Monsignor Gervais Banshimiyubusa Receives The Pallium From Pope Francis" (Translated from the original French language). Roman Catholic Archdiocese of Bujumbura. Bujumbura, Burundi. Iliwekwa mnamo 19 Februari 2025.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
| Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |