Gertrude Mongella

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Gertrude Mongella

Gertrude Ibengwe Mongella alikuwa Rais wa kwanza wa Bunge la Umoja wa Afrika. Pia alikuwa mbunge wa jimbo la Ukerewe katika bunge la taifa nchini Tanzania.[1] Anatokea katika chama cha CCM.

Gertrude alizaliwa mwaka 1945 katika kisiwa cha Ukerewe katika Mkoa wa Mwanza (Tanzania). Baba yake, Patrice Magologozi alikuwa fundi seremala na mwashi na mama yake, Bibi Nambona, alikuwa mkulima.

Gertrude Mongela ameshika nyadhifa mbalimbali za kitaifa na kimataifa. Miaka 1993-1995 alikuwa Katibu Mkuu wa Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Masuala ya Wanawake na kuhudhuria mkutano wake wa nne uliofanyika Beijing, China mwaka 1995. Amewahi kuwa balozi nchini India (1991-1993), Waziri Asiye na Wizara Maalum, Waziri wa Ardhi, Maliasili na Utalii, mshauri maalum wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi, na Utamaduni,[2] n.k.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "Mengi kuhusu Getrude Ibengwe Mongella". 25 Aprili 2006. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2012-05-21. Iliwekwa mnamo 11 Novemba 2011. 
  2. "africanfront.org(AUF)". www.africanfront.org. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-09-21. Iliwekwa mnamo 2020-08-21. 

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]