Gertrud Adelborg

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Agda Montelius na Gertrud Adelborg akiwasilisha ombi la mwanamke kujiandikisha kwa Waziri Mkuu Erik Gustaf Boström mnamo 1899.

Gertrud Virginia Adelborg (Karlskrona, 10 Septemba 185325 Januari 1942) alikuwa mwalimu, mwanaharakati wa mshiriki mkuu wa harakati za haki za wanawake wa nchini Uswidi. [1]

Wasifu[hariri | hariri chanzo]

Gertrud Adelborg alizaliwa Karlskrona katika Kaunti ya Blekinge, Uswidi. Alikuwa binti wa Nahodha mashuhuri wa wanamaji Bror Jacob Adelborg (1816-1865) na mkewe Hedvig Catharina af Uhr (1820 -1903). Alikuwa dada wa mchoraji wa vitabu Ottilia Adelborg (18551936) na msanii wa nguo Maria Adelborg (1849-1940). Hakuwahi kuolewa. Adelborg alisomeshwa katika shule za wasichana. Alifanya kazi kama mwalimu mnamo 187479, na aliajiriwa katika Mahakama ya Rufaa ya Svea (Kiswidi: Svea hovrätt ) kuanzia mwaka 188183.

Gertrud Adelborg alikuwa mtendaji ndani ya harakati za wanawake ( woman suffrage) nchini Uswidi. Alifanya kazi katika ofisi ya Chama cha Fredrika Bremer Association au FBF mnamo 1884-1907 (tangu 1886 kama mwenyekiti wa ofisi ya Stockholm) na alikuwa mwanachama wa Jumuiya kuu ya FBF mnamo 1897-1915. Alianzisha Shule ya Wanawake ya FBF ((Kiswidi: Landthushållningsskola för kvinnor ) huko Östergötland ambapo alikuwa mshiriki wa bodi ya shule mnamo 1907-1921.

Mnamo mwaka wa 1899, wajumbe kutoka FBF waliwasilisha pendekezo la mwanamke kupata kura kwa Waziri Mkuu Erik Gustaf Boström . Ujumbe huo uliongozwa na Agda Montelius, akiandamana na Gertrud Adelborg, ambaye alikuwa ameandika ombi hilo. Hii ilikuwa mara ya kwanza kwa harakati za wanawake wa Uswidi wenyewe kuwasilisha hitaji la haki ya kupiga kura.

Vyanzo[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "Gertrud Adelborg". WordPress. Iliwekwa mnamo December 1, 2018.  Check date values in: |accessdate= (help)
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Gertrud Adelborg kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.