Geronimo Rulli
| Gerónimo Rulli | |
| Amezaliwa | Gerónimo Rulli 20 Mei 1992 La Plata, Argentina |
|---|---|
| Nchi | Argentina |
| Urefu | 1.89 m |
Gerónimo Rulli (alizaliwa 20 Mei 1992) ni mchezaji wa mpira wa miguu wa kulipwa kutoka nchini Argentina anayecheza nafasi ya golikipa katika klabu ya Manchester City inayoshiriki ligi kuu nchini Uingereza na timu ya taifa ya Argentina.
Rulli alijiunga na timu ya vijana ya Estudiantes mnamo mwaka 2009, na akacheza mechi yake ya kwanza ya kulipwa klabuni hapo mnamo mwaka 2013. Baina ya mwaka 2014 na 2020, alicheza katika klabu ya Real Sociedad ya nchini Uhispania, kwanza kwa mikataba miwili ya mkopo kabla ya kusajiliwa jumla mnamo mwaka 2017. Alicheza mechi 170 katika misimu mitano klabuni hapo. Mnamo mwaka 2019, alijiunga na klabu ya Montpellier ya Ufaransa kwa mkopo. Mnamo mwaka 2020, alijiunga na Villarreal na kudumu klabuni hapo kwa misimu miwili na nusu, akitwaa ubingwa wa Ligi ya ulaya ya UEFA katika msimu wa 2020–21.[1]
Alicheza katika timu ya taifa ya Argentina kwenye mashindano ya Olimpiki ya mwaka 2016 nchini Brazil. Alicheza mechi yake ya kwanza katika timu ya wakubwa mnamo mwaka 2018. Ingawa hakucheza dakika yoyote, Rulli alikuwa sehemu ya vikosi vya Argentina vilivyotwaa ubingwa wa Kombe la Dunia la FIFA la mwaka 2022 na Copa Amerika 2024. Pia aliiwakilisha Argentina katika Michezo ya Olimpiki ya mwaka 2024.[2]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Geronimo Rulli - National Football Teams". National Football Teams. Iliwekwa mnamo 19 Septemba 2026.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "RULLI Geronimo". Paris 2024 Olympics. Iliwekwa mnamo 19 Septemba 2026.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
| Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Geronimo Rulli kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |