Jeromu Emiliani

Jeromu Emiliani (Venisi, Italia, 1486 – Somasca, karibu na Bergamo, 8 Februari 1537) alikuwa padri na mwanzilishi wa utawa nchini Italia.
Papa Klementi XIII alimtangaza mtakatifu mwaka 1767, halafu Papa Pius XI alimtangaza msimamizi wa mayatima mwaka 1928.
Sikukuu yake ni tarehe 8 Februari[1].
Maisha
[hariri | hariri chanzo]Kwanza alikuwa askari, akitumia ujana wake katika anasa na ukatili, lakini baada ya kutupwa gerezani na maadui wake, alimuongokea Mungu akaacha kazi hiyo akawapa fukara mali yake yote ili ajitoe mhanga pamoja na wenzake kadhaa kuwahudumia maskini, hasa mayatima na wagonjwa [2].
Baada ya kupata upadri (1518) alianzisha kwa ajili hiyo shirika la wakleri walioitwa Wasomaska.
Wakati wa kuhudumia wenye tauni, aliambukizwa nao akafariki kwa ugonjwa huo wa kutisha.
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]Marejeo ya Kiswahili
[hariri | hariri chanzo]- Masomo ya Breviari - Sikukuu za Bwana, za Bikira Maria na za Watakatifu - Ndanda Mission Press 1978, uk 57-59
- John Kabeya na wengine - Maisha ya Watakatifu – ed. T.M.P. Book Department – Tabora 1965, 1989, uk. 48-49
- Pd. Leandry Kimario, O.F.M.Cap. - Mfahamu Mtakatifu Somo Wako - Maisha ya Watakatifu wa Kila Siku pamoja na Watakatifu Wafransisko - Toleo la pili - Dar es Salaam 2021, uk. 39-40
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- "St. Jerome Emiliani". Catholic Encyclopedia.
- Sanamu yake kama mwanzilishi katika Basilika la Mt. Petro (Vatikani).
| Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |