Gerard Deulofeu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Gerard Deulofeu

Gerard Deulofeu (alizaliwa 13 Machi 1994) ni mchezaji wa soka wa Hispania ambaye anacheza kama mshambuliaji na pia kama winga katika klabu ya Ligi Kuu ya Uingereza ya Watford F.C na Timu ya taifa ya Hispania.

Kazi ya klabu[hariri | hariri chanzo]

Everton[hariri | hariri chanzo]

Deulofeu alijiunga na klabu ya Everton kabisa mnamo 1 Julai 2015, kwa ada ya uhamisho iliyoripotiwa kuwa £ 4.2 milioni. Alifunga goli lake la kwanza kama mchezaji wa kudumu wa Everton katika ushindi wa 2-1 dhidi ya klabu ya Reading katika mzunguko wa tatu ya Kombe la Ligi.

Kurudi ya Barcelona[hariri | hariri chanzo]

Mnamo tarehe 30 Juni 2017, Deulofeu alirudi Barcelona,Mnamo tarehe 21 Oktoba, alifunga goli lake la kwanza kwa klabu hiyo katika dakika ya 2 kwa ushindi wa 2-0 dhidi ya klabu ya Málaga.

Watford F.C.[hariri | hariri chanzo]

Tarehe 29 Januari 2018, ilitangazwa kuwa Deulofeu amejiunga na Watford F.C kwa mkataba wa mkopo hadi mwisho wa msimu.Mnamo tarehe 5 Februari 2018, alifunga goli lake la kwanza na Watford kupata ushindi wa magoli 4-1 dhidi ya Chelsea katika mchezo wa Ligi Kuu ya Uingereza.

Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Gerard Deulofeu kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.