Nenda kwa yaliyomo

Geoff Hurst

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Sir Geoff Hurst

Amezaliwa 8 Desemba 1941 (1941-12-08) (umri 84)
Ashton-under-Lyne, England
Urefu 1.82 m

Sir Geoffrey Charles Hurst (alizaliwa 8 Desemba 1941) ni mchezaji wa zamani wa mpira wa miguu wa kulipwa kutoka nchini Uingereza. Akiwa mshambuliaji, alikuwa mchezaji wa kwanza kufunga mabao matatu katika mechi moja kwenye fainali ya kombe la dunia la FIFA, wakati Uingereza ilipoibuka na ushindi wa mabao 4–2 dhidi ya Ujerumani Magharibi katika Uwanja wa Wembley mwaka 1966.

Hurst alianza taaluma yake akiwa na klabu ya West Ham United, ambapo alifunga mabao 242 katika mechi 500 za timu ya kwanza. Akiwa hapo, alishinda Kombe la FA mwaka 1964 na Kombe la Washindi la Ulaya mwaka 1965. Aliuuzwa kwenda Stoke City mwaka 1972 kwa pauni 80,000. Baada ya msimu mitatu akiwa na Stoke, ambapo alishinda Kombe la Watney mwaka 1973,[1] alimaliza taaluma yake ya Ligi ya Soka nchini Uingereza akiwa na West Bromwich Albion mwaka 1976. Hurst alienda kucheza soka nchini Ireland katika klabu ya Cork Celtic na Marekani kwenye klabu ya Seattle Sounders, kabla ya kurejea Uingereza kuifundisha klabu isiyo ya ligi kuu ya Telford United. Pia alikuwa kocha katika benchi la ufundi la timu ya taifa ya Uingereza kabla ya kuhudumu kwa miaka miwili kama kocha wa Chelsea kuanzia mwaka 1979 hadi 1981. Baadaye aliifundisha klabu ya Kuwait SC, kabla ya kuacha mambo ya mpira ili kuangazia biashara zake.

Kwa ujumla, Hurst alifunga mabao 24 katika mechi 49 alizochezea Uingereza, na mbali na mafanikio ya Kombe la Dunia la mwaka 1966, pia alicheza katika mashindano ya Euro mwaka 1968 na kombe la dunia la FIFA la mwaka 1970. Pia alikuwa na taaluma fupi ya mchezo wa kriketi, akiichezea klabu ya Essex mechi moja ya daraja la kwanza mwaka 1962, kabla ya kuwekeza nguvu zake zote kwenye mpira wa miguu.

  1. "Stoke City And The Watney Cup". World Football Index. 18 Agosti 2018. Iliwekwa mnamo 25 Juni 2022.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Geoff Hurst kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.