Gennady Abramov
Gennady Abramov alikuwa msimamizi wa Muungano wa Wakristo Waevanjeli ya Baptisti wa Urusi (UECB) katika Mashariki ya Mbali ya Urusi.
Wasifu
[hariri | hariri chanzo]Mchungaji Gennady Abramov alikuwa makamu wa rais wa kikanda UECB katika mashariki ya mbali ya Urusi,iliyoko Khabarovsk. Alikuwa na huduma ya Uinjilisti wa kusafiri, akitembea katika eneo hilo kubwa akiwahamasisha wamisionari wa kitaifa na kusaidia kuendeleza makanisa.[1] Mwaka 1992 eneo lenye watu milioni 10 lilikuwa na makanisa ya kibaptisti yasiyozidi 20, na makanisa hayo yalikuwa yamechakaa yalihitaji ukarabati. Jumla ya waamini waliobatizwa katika eneo hilo walikuwa chini ya 2,500. Hata hivo Ambramov alikuwa na matumain ya kukusanya fedha ili kujenga kituo cha kiroho cha Mashariki ya mbali mjini Khabarovsk,chenye ukumbi wenye viti 600 pamoja na miundombinu ya kufundishia wachungaji na walimu wa shule ya jumapili kutoka sehemu zote za mashariki ya mbali.[2] Makanisa katika eneo hilo yalikuwa yakiripoti ukuaji wa hatua kwa hatua ambapo watu 423 walibatizwa mwaka 1991.
Katika mahojiano ya mwaka 1997, mmisionari wa Southern Baptist aliyekuwa akitembelea eneo hilo Wayne Kennston, amabye anafanya kazi karibu na Ambramov alisema " Miaka minne iliyopita huenda kulikuwa na makanisa 24 ya Kibaptisti katika mashariki ya mbali ya Urusi . Sasa yapo zaidi ya 60. Mwaka 1998 Abramov alihudhuria mkutano wa wa mwaka wa Alaska Baptist Connvention, ambapo ushirikiano wa miaka mitatu kati ya wabaptisti wa Alaska na wa mashariki ya mbali ya Urusi ulizinduliwa [3]
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "A 2,000 Mile Pauline Journey" (PDF). InSight. Slavic Gospel Association. Januari 2010. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2011-07-06. Iliwekwa mnamo 2010-08-27.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Trennis Henderson (Juni 8, 1992). "Baptist medical team evaluates medical technology in Russia" (PDF). Baptist Press. Iliwekwa mnamo 2010-08-27.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Alaskan Baptists undertake Far East Russian partnership". Baptist Press. Sep 1, 1998. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2012-03-06. Iliwekwa mnamo 2010-08-27.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
| Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |