Gaudensi wa Novara
Mandhari
Gaudensi wa Novara (Ivrea, Piemonte, Italia, 327 - Novara, 3 Agosti 418) alikuwa askofu wa kwanza wa jimbo la Novara, Italia Kaskazini mwishoni mwa karne ya 4 hadi mwanzoni mwa karne ya 5.
Mzaliwa wa familia ya Kipagani, inasemekana aliongokea Ukristo kwa msaada wa Eusebi wa Vercelli ambaye baadaye alimpa upadrisho.
Baadaye tena alisaidiwa na Ambrosi katika utume wake, na kufanywa askofu (397) na Simplicianus, mwandamizi wa Ambrosi.
Heshima ya watu kwake kama mtakatifu ni ya zamani sana.
Sikukuu yake huadhimishwa kila mwaka tarehe 22 Januari[1].
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]- Watakatifu wa Agano la Kale
- Orodha ya Watakatifu Wakristo
- Orodha ya Watakatifu wa Afrika
- Orodha ya Watakatifu Wafransisko
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- Nicholas Everett, Patron Saints of Early Medieval Italy AD c.350-800 (PIMS/ Durham University Press, 2016), pp.14-38.
- Nicholas Everett, "The Hagiography of Lombard Italy", Hagiographica 7 (2000) 92-100.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |