Nenda kwa yaliyomo

Gamal Nkrumah

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kijana Gamal (aliyesimama mbele ya Rais wa Misri Gamal Abdel Nasser, aliyesimama wa tatu kutoka kushoto) na familia yake, 1965. Baba yake Kwame Nkrumah (wa kwanza kulia)

Gamal Gorkeh Nkrumah (amezaliwa 1958) ni mwandishi wa habari kutoka Ghana, Pan-Africanist na mhariri wa gazeti la Al Ahram Weekly. Ndiye mwana wa kwanza wa rais wa Ghana wa kwanza, Kwame Nkrumah,[1] na mke wake Mmisri, Fathia Nkrumah.

Gamal Nkrumah alipata shahada ya uzamili katika sayansi ya siasa kutoka Shule ya Mafunzo ya Mashariki na Afrika mjini London. Kwanza aliwahi kufanya kazi kama mwandishi wa siasa katika Al-Ahram Weekly huko Cairo[1] kwa zaidi ya miaka 15. Hivi sasa, yeye ni mhariri wa idara ya masuala ya kimataifa katika gazeti hilo.

  1. 1 2 Ceesay, Fabakary B. (1 Oktoba 2007). "Watoto wa Nkrumah Wataendeleza Urithi wa Baba yao". Foroyaa online. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 21 Julai 2011. Iliwekwa mnamo 15 Januari 2010.

Viungo vya Nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Gamal Nkrumah kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.