Gabriel Ruhumbika

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Gabriel Ruhumbika (alizaliwa katika kisiwa cha Ukerewe, 1938) ni mwandishi, mtafsiri na mtaaluma kutoka Tanzania anayeishi nchini Marekani akiwa profesa wa University of Georgia.

Ruhumbika huandika hadithi fupifupi. Riwaya yake ya kwanza, iitwayo Village in Uhuru, ilichapishwa mnamo mwaka 1969. Aliandika riwaya mbalimbali kwa mfuatano kwa kutumia lugha ya Kiswahili.

Pia alifundisha fasihi katika vyuo vikuu mbalimbali, na kwa sasa ni muadhiri katika chuo kikuu cha maandishi ya kulinganisha (uandishi wa kulinganisha) cha Georgia nchini Marekani

Maisha yake ya awali[hariri | hariri chanzo]

Ruhumbika alizaliwa Ukerewe, ndani ya ziwa Viktoria. Baada ya kumaliza masomo ya shahada yake ya kwanza katika chuo cha Makerere University nchini Uganda, pia alimaliza shahada ya uzamivu kuhusu Fasihi ya Kiafrika katika Chuo kikuu cha Paris-Sorbonne nchini Ufaransa.

Machapisho yake[hariri | hariri chanzo]

  • Village in Uhuru, 1969[1]
  • Miradi Bubu ya Wazalendo, 1991[2]
  • Janga Sugu la Wazawa, 2002[3]

Taaluma[hariri | hariri chanzo]

Riwaya ya kwanza ya Ruhumbika, "Village in Uhuru[dead link]", ilichapishwa mnamo mwaka 1969; Hii ilikuwa riwaya ya pili ya lugha ya kiiingereza katika nchi ya Tanzania, Baada ya ile ya Peter Palangyo "Dying in the sun" (1968).). Hii ni riwaya ya historia, ambayo iliegemea zaidi upande wa matukio halisi yanayoendana na maswala ya maadili na utambulisho wa taifa katika kulingana na Tanganyika African National Union (TANU) katika kupambania uhuru wa Tanganyika (sasa Tanzania). Ingawa "Village in Uhuru" Aliandika na alichapisha kwa mara ya kwanza kwa kiingereza, Ruhumbika aliamua kuandika riwaya zake zote zilizofuata kwa lugha ya kiswahili, maamuzi ambayo yalikuwa sawa na mwandishi kutoka kenya Ngũgĩ wa Thiong'o.

Riwaya zake ziliandikwa kwa lugha ya Kiswahili, ambazo zilibeba hasa jarida Pan-African Uhuru Movement, Jumuisha "Miradi Bubu ya Wazalendo" (Invisible Enterprises of the Patriots, 1991) na " Janga Sugu la Wazawa" (Everlasting Doom for the Children of the Land, 2002). Pia aliandika kusanyiko la hadithi fupi, "Uwike Usiwike Kutakuche"(Whether the Cock Crows or Not It Dawns).

Mbali ya kuwa mwandishi pia alikuwa mtafsiri, hasa maneno kutoka lugha ya kifaransa kwenda lugha ya kiswahili, Ingawa alitafsiri pia riwaya katika Aniceti Kitereza's "Mnyombekere na mkewe Bugonoka, na kijana wao wa kiume Ntulanalwo, na binti yao Bulihwali" kutoka Kikerewe kwenda Kiingereza.

Ruhumbika, pia alifundisha fasihi katika vyuo vikuu tofauti tofauti, sehemu zote Africa na Marekani (USA). Alikuwa mkufunzi katika chuo kikuu cha Dar es Salaam (kutoka 1970 hadi 1985) na Chuo kikuu cha Hampton katika mji wa Virginia (kutoka 1985 hadi 1992). Tangu 1992, Alikuwa profesa wa uandishi wa fasihi za kulinganisha katika Chuo kikuu cha Georgia.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Conor McGlacken (2015-06-29). "Village in Uhuru". The Groundnut (kwa en-US). Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-12-28. Iliwekwa mnamo 2019-12-28. 
  2. Ruhumbika, Gabriel (1995). Miradi bubu ya wazalendo (kwa Kiswahili). Tanzania Publishing House. ISBN 978-9976-1-0176-8. 
  3. "9789987622313: Janga Sugu La Wazawa - AbeBooks - GABRIEL RUHUMBIKA: 9987622313". www.abebooks.com (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2019-12-28. 
Makala hii kuhusu mwandishi fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Gabriel Ruhumbika kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.