Nenda kwa yaliyomo

Fundisanifu wa uhandisi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Fundisanifu wa uhandisi ni mtaalamu aliyefunzwa ujuzi na mbinu zinazohusiana na tawi mahususi la teknolojia ya uhandisi, akiwa na uelewa wa vitendo wa dhana husika za uhandisi. Mkataba wa Dublin uliotiwa saini mwaka wa 2002 ni mkataba wa kimataifa unaotambua sifa za ufundisanifu wa uhandisi.

Nchini Kenya na Tanzania, fundisanifu huwa ni mtu aliyehitimu stashahada ya teknolojia ya uhandisi katika chuo cha ufundi[1][2].

Majukumu ya fundisanifu

[hariri | hariri chanzo]

Fundisanifu huhusika katika kazi mbalimbali za kiuhandisi na ufundi ikiwemo:

  • Kujenga
  • Kukarabati
  • Kusakinisha mitambo
  • Kufanya majaribio
  • Kukusanya data na kuikokotoa
  • Usanifu wa michoro ya kiuhandisi
  1. Engineering Technology Act (kwa Kiingereza). 2022-12-31.
  2. "ENGINEERS REGISTRATION ACT - Laws of Tanzania". tanzanialaws.com. Iliwekwa mnamo 2025-08-22.