Nenda kwa yaliyomo

Fukuzawa Yukichi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Fukuzawa Yukichi (福澤 諭吉, 10 Januari 18353 Februari 1901) alikuwa mwalimu, mwanafalsafa, mwandishi, mjasiriamali na askari wa Japani. Alianzisha Chuo cha Keio Gijuku, gazeti la Jiji-Shinpō, na Taasisi ya Magonjwa ya Kuambukiza.

Alitetea mageuzi wakati wa kipindi cha Meiji, na mawazo yake yaliathiri sana serikali na jamii ya Japani. Picha yake ilionekana kwenye noti ya Yen 10,000 kuanzia 1984 hadi 2024.[1][2][3][4][5][6][7]

Fukuzawa Yukichi alizaliwa mwaka 1835 katika familia ya askari wa cheo cha chini katika Ukoo wa Okudaira, Nakatsu (sasa Ōita, Kyushu). Familia yake iliishi Osaka, kituo cha biashara cha Japani kwa wakati huo. Baada ya baba yake kufariki mapema,akiwa na miaka 5 alianza kujifunza maandiko ya Kichina, na kufikia miaka 14 alikuwa anasoma vitabu vikubwa vya falsafa. Alivutiwa sana na mwalimu wake Shōzan Shiraishi.

Mnamo 1854, baada ya Wamarekani kufika Japani, Fukuzawa alianza kujifunza Kiholanzi ili kuelewa sayansi na silaha za Ulaya. Alisoma katika shule ya Tekijuku ya Ogata Kōan, ambapo alijua Kiholanzi vizuri. Mwaka 1858 akawa mwalimu wa lugha hiyo.

Alipogundua kuwa wafanyabiashara wa Ulaya walitumia Kiingereza zaidi ya Kiholanzi, akaanza kujifunza Kiingereza licha ya changamoto za vitabu na kamusi chache.

  1. "Security Features of Bank of Japan Notes- 10,000 yen Note (Shotoku Taishi), 5,000 yen Note (Shotoku Taishi), 1,000 yen Note (Hirobumi Ito) and 500 yen Note (Tomomi Iwakura) - : 日本銀行 Bank of Japan". Bank of Japan (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2025-01-03.
  2. Kigezo:Harvtxt
  3. Hopper, Helen M. (2005). Fukuzawa Yukichi : from samurai to capitalist. New York: Pearson/Longman. ISBN 978-0321078025. OCLC 54694712.
  4. 森田, 康夫 (1996). 福沢諭吉と大坂 (kwa Kijapani). 和泉書院. uk. 126. ISBN 978-4-87088-820-3. ウェーランドの『モラル・サイヤンス』( F.Wayland : The Element of Moral Science)の影響は、その意味からも福沢思想にとって決定的意義をもっていた。
  5. Métraux, Daniel A. (2011). "Democratic Trends in Meiji Japan". Association for Asian Studies (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2024-01-12.
  6. Isomura, Yukio; Sakai, Hideya (2012). (国指定史跡事典) National Historic Site Encyclopedia. 学生社. ISBN 978-4311750403.(in Japanese)
  7. "福沢諭吉旧居" (kwa Japanese). Agency for Cultural Affairs. Iliwekwa mnamo Agosti 20, 2020.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) CS1 maint: unrecognized language (link)
Makala hii kuhusu mwandishi fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Fukuzawa Yukichi kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.