Fridolin Ambongo Besungu
Mandhari
Fridolin Ambongo Besungu, OFM Cap. (alizaliwa 24 Januari 1960) ni kardinali wa Kanisa Katoliki kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ambaye amekuwa Askofu Mkuu wa Kinshasa tangu mwaka 2018.
Alikuwa Askofu wa Bokungu-Ikela kuanzia mwaka 2004 hadi 2016, Msimamizi wa Kitume wa Kole kuanzia mwaka 2008 hadi 2015, Askofu Mkuu wa Mbandaka-Bikoro kuanzia mwaka 2016 hadi 2018, Msimamizi wa Kitume wa Bokungu-Ikela kuanzia mwaka 2016 hadi 2018, na Askofu Mkuu Msaidizi wa Kinshasa mwaka 2018. Yeye ni mwanachama wa Shirika la Wafransisko Wakapuchini.[1]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ MacDonald, G. Jeffrey (5 Juni 2018). "Church suspends sacraments as deadly Ebola outbreak spreads". National Catholic Reporter. Iliwekwa mnamo 1 Novemba 2018.
{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
| Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |