Freshta Karim
Freshta Karim (amezaliwa Kabul, 5 Aprili 1992) ni mwanaharakati wa haki za watoto na mtangazaji wa televisheni kutoka Afghanistan. Yeye ni mwanzilishi na mkurugenzi wa Charmaghz, NGO yenye makao yake Kabul inayojitolea kukuza elimu ya watoto nchini Afghanistan.
Maisha ya awali na kazi
[hariri | hariri chanzo]Karim alizaliwa takribani wiki tatu kabla ya kuanza kwa Vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Afghanistan. Alitumia maisha yake ya awali nchini Pakistan kama mkimbizi kabla ya kurejea Kabul. Akiwa na umri wa miaka 12, aliwasiliana na kituo cha televisheni cha eneo hilo na kuajiriwa kama mtangazaji wa kipindi ambacho kilicholenga watoto. Wakati wa ujana wake, alifanya kazi katika vituo mbalimbali vya redio na televisheni vya ndani.
Karim alisomea Political Science katika Panjab University, kisha akakamilisha shahada ya uzamili katika sera ya Umma katika chuo kikuu cha University of Oxford .
Baada ya kukamilisha masomo yake mwaka 2017, Karim alirejea Afghanistan. Mwaka 2018, alianzisha NGO, Charmaghz,[1] kwa lengo la kukuza elimu, ujuzi wa kusoma na kuandika, pamoja na fikra makini kwa watoto, katika nchi iliyoathiriwa na miongo kadhaa ya vita. Shirika hilo hubadilisha mabasi ya umma yasiyotumika kuwa maktaba zinazotembea, ambapo watoto hujifunza kusoma na kuandika, kushiriki katika shughuli za kisanii, na kusikiliza hadithi.[2]
Baada ya Kuanguka kwa Kabul mwezi Agosti 2021, Karim aliomba hifadhi ya kisiasa nchini Uingereza, ambako kwa sasa anaishi. Tarehe 17 Novemba 2021, Karim alihutubia baraza la usalama la umoja wa mataifa ambapo alisema: “Tunahitaji kufanya juhudi kumwona mwanadamu ndani ya wengine, kusikia mateso yao na hadithi zao…Leo ninaanza safari hii kwa kutangaza kwamba hakuna mtu aliye adui.”[3]
Hadi mwaka 2023, Karim alihudumu kama mshauri mwandamizi wa Malala Fund.[4] Mwaka 2023, alichaguliwa kuwa mjumbe wa bodi ya BBC Media Action.[5]
Tuzo na utambuzi
[hariri | hariri chanzo]Mwaka 2019, Karim alitunukiwa Max-Herrmann-Preis,[6] na pia aliorodheshwa na jarida la Forbes katika orodha ya vijana wenye umri chini ya miaka 30 amabao wameonyesha ubunifu,uongozi na mafanikio makubwa .[7] Mwaka 2021, aliorodheshwa na shirika la BBC ikimtaja mmoja wa wanawake 100 mwenye ushawishi katika jamii,[8] na alikuwa mmoja wa washindi wa mwisho wa Sakharov Prize ya Bunge la Ulaya[9] (iliyotolewa mwaka huo kwa Alexei Navalny), pamoja na wanawake wengine kumi kutoka Afghanistan.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Charmaghz Executive Team". Charmaghz.org. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 26 Septemba 2023. Iliwekwa mnamo 26 Septemba 2023.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Mobile Libraries". Charmarghz.org. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 26 Septemba 2023. Iliwekwa mnamo 26 Septemba 2023.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Alumna Freshta Karim addresses UN Security Council on Afghanistan Conflict". www.some.ox.ac.uk. 3 Desemba 2021. Iliwekwa mnamo 26 Septemba 2023.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Karim, Freshta (7 Machi 2022). "Freshta Karim on how to change the lives of Afghanistan's women". assembly.malala.org. Iliwekwa mnamo 2024-10-03.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Freshta Karim". www.bbc.co.uk. Iliwekwa mnamo 26 Septemba 2023.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Max-Herrmann-Preis 2019 an Freshta Karim (Kabul) und Bara'a Al-Bayati (Bagdad)". www.freunde-sbb.de.
- ↑ "Freshta Karim". www.forbes.com. Iliwekwa mnamo 26 Septemba 2023.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "BBC 100 Women 2021: Who is on the list this year?". BBC News. 7 Desemba 2021. Iliwekwa mnamo 26 Septemba 2023.
{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Sakharov Prize 2021: the finalists". www.europarl.europa.eu. 14 Oktoba 2021. Iliwekwa mnamo 26 Septemba 2023.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)