Fransisko Solano


Fransisko Solano, O.F.M. (jina la Kihispania kwa kirefu lilikuwa: Francisco Sánchez-Solano Jiménez; Montilla, Córdoba, Andalusia, Hispania, 10 Machi 1549 - Lima, Peru, 14 Julai 1610) alikuwa mtawa wa urekebisho wa Wareformati wa shirika la Ndugu Wadogo na padri wa Kanisa Katoliki. kutoka Hispania na mmisionari huko Amerika Kusini.
Alifanya kazi ya kuhubiri na kueneza imani ya Kikristo katika maeneo mbalimbali ya Amerika Kusini, akijulikana kwa ufanisi wake wa kiroho na huruma kwa wahitaji.[1]
Ili kuokoa watu alifanya umisionari katika nchi mbalimbali za Amerika Kusini, akihubiri na kutoa ushuhuda wake kwa Waindio na kwa wakoloni pia upya wa maisha ya Kikristo[2].
Papa Klementi X alimtangaza mwenye heri tarehe 20 Juni 1675, halafu Papa Benedikto XIII alimtangaza mtakatifu tarehe 27 Desemba 1726.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 14 Julai[3].
Sala yake
[hariri | hariri chanzo]Yesu mwema, mkombozi na rafiki yangu!
Nina kitu gani usichonipa wewe? Najua nini usiyonifundisha wewe?
Nina thamani gani usipokuwa nami?...
Ndiwe uliyeniumba, tena bila ya kuniuliza. Wewe umeniumba.
Elekeza macho yako kwangu, Bwana, na unihurumie, kwa kuwa mimi ni mkiwa na maskini...
Kwa nini, Bwana Yesu wangu, wewe umesulubiwa, nami nasaidiwa na watumishi wako?
Kwa nini wewe uchi, nami nina vazi?
Kwa nini wewe umepigwa makofi na kutiwa taji la miba, nami nimepewa vitu vyema na kufarijiwa na fadhili nyingi?...
Mungu wa roho yangu, utukuzwe kwa yale uliyonijalia!
Bwana wangu, nafurahi kwamba u Mungu; jinsi hilo lilivyo zuri!
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]- Watakatifu wa Agano la Kale
- Orodha ya Watakatifu Wakristo
- Orodha ya Watakatifu wa Afrika
- Orodha ya Watakatifu Wafransisko
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Donovan, Stephen (1909). "Kigezo:Cite wikisource/make link". Catholic Encyclopedia. Juz. la 6.
- ↑ https://www.santiebeati.it/dettaglio/62600
- ↑ Martyrologium Romanum
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Francis Solano Ilihifadhiwa 4 Juni 2012 kwenye Wayback Machine. at Patron saints Index Ilihifadhiwa 29 Agosti 2013 kwenye Wayback Machine.
- St. Francis Solano Ilihifadhiwa 15 Agosti 2007 kwenye Wayback Machine. at "Saints Alive"
- (Kihispania) San Francisco Solano Ilihifadhiwa 17 Juni 2012 kwenye Wayback Machine.
![]() |
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |