Franka Potente
Franka Potente | |
---|---|
Franka Potente, 2019 | |
Amezaliwa | 22 Julai 1974 Münster, Rhine Kaskazini-Westfalia, Ujerumani |
Franka Potente (amezaliwa tar. 22 Julai 1974) ni mwigizaji wa filamu kutoka nchini Ujerumani. Alianza kuonekana kwa mara ya kwanza katika vichekesho vya It's a Jungle Out There (1995) na kuanza kupata kutambulika zaidi baada ya kucheza katika filamu ya kutisha ya Lola Rennt (ambayo pia ilitolewa kwa Kiingereza kama Run Lola Run) (1998).
Baada ya kukaa takriban miaka mitano ya umaarufu wa filamu za Kijerumani, Potente akapata mwamko wa filamu za huko Hollywood baada ya kupata kucheza kama Barbara Buckley katika filamu ya Blow (2001) na vilevile kucheza kama mshiriki mwandamizi wa Matt Damon katika filamu ya The Bourne Identity (2002).
Potente amepata tuzo chungu mzima za filamu na televisheni za Kijeruamani kwa kuwa mwigizaji bora wa filamu ya Run Lola Run na Opernball. Potente amepata kushirki katika sehemu za uhusika mkuu katika filamu kadhaa za bajeti ndogo, zikiwemo filamu za kutisha, mapenzi, vichekesho, uzushi wa kisayansi, maigizo, na filamu za kupigana.
Wasifu
[hariri | hariri chanzo]Maisha ya awali
[hariri | hariri chanzo]Yeye n mkubwa katika familia ya watoto wawili, Potente alizaliwa mjini Münster,[1] Rhine Kaskazini-Westfalia, na kukulia karibu katika eneo lililo karibu na Dülmen.[2]
Mama yake, Hildegard, ni msaidizi wa kutoa dawa kwa wagonjwa, na baba yake, Dieter Potente, ni mwalimu.[3] Jina la mzee wake linatokana na asili ya Kitaliano, yaani babu yake mkuu anatokea huko, ambaye alihamia Ujerumani kunako maiaka ya 1800.
Akiwa na umri wa miaka 17, alitumia muda kadhaa akiwa kama mwanafunzi huko mjini Texas.[4]
Shughuliza sanaa
[hariri | hariri chanzo]Baada ya kumaliza masomo yake nchini Ujerumani, akajiandikisha katika Chuo cha Sanaa cha Otto Falckenberg cha mjini Munich. Potente akawa anafanya kazi za uigizaji nje ya muda wa shule na alianza kuonekana kwa mara ya kwanza katika filamu mwaka wa 1995 katika filamu ya mwanafunzi ya Aufbruch.
Baada ya hapo akaja kuigiza kama kachero katika filamu ya Nach Fünf im Urwald (It's a Jungle Out There), ambayo aliiongoza yeye na bwana wake, Hans Christian Schmid. Kunako mwaka wa 1995 alipata Tuzo ya Bavaria kwa Vijana Wenyevipaji kwa kuigiza vyema katika filamu zake. Halafu baadaye akaja kumalizia mwaka wake wa mwisho wa mafunzo katika Taasisi ya Maigizo ya Lee Strasberg ya mjini Manhattan.
Baadaye Potente akarudi zake Ulaya na kuja kufanya kazi katika filamu za Kijerumani na Kifaransa. Alipata kucheza kama mhusika mkuu katika filamu ya Lola Rennt (Run Lola Run) ni baada ya kuonana na mwongozaji, Tom Tykwer, katika mgahawa. Uhusika huo uliandikwa kwa ajili yake japokuwa filamu ilikuwa ya bajeti ndogo, na filamu ilitengenezwa na Art house film production, ambayo ilikuwa maarufu sana katika Ulaya.
Franka Potente pia alishawahi kushiriki katika utengenezaji wa vibwagizo. Ameshiriki katika filamu nyingi za lugha ya Kijerumani, ikiwa pamoja na filamu za kutisha, Anatomy na filamu nyingine ya kutisha ya mapenzi maarufu kama The Princess and the Warrior.
Alianza kushiriki kwa mara ya kwanza katika filamu za lugha ya Kiingereza, ni baada ya kuwa kama mhadithiaji katika filamu ya Storytelling mnamo mwaka wa 2001. Baada ya hapo ikafuatiwa na filamu ya Blow, ambayo kacheza na Johnny Depp, na pia kuwa kama mshiriki mwandamizi wa katika filamu ya The Bourne Identity, akiwa sambamba kabisa na Matt Damon, ambayo pia aliendelea hadi katika sehemu ya pili yake ya The Bourne Supremacy.
Mnamo mwaka wa 2006, alishirikiana na Eric Bana katika filamu ya Kiaustralia ya Romulus, My Father, ambayo ilimwezesha kupata Tuzo ya Kiaustralia kwa kuwa kama mwigizaji bora wa kike. Na pia mnamo mwaka huohuo wa 2006, alitunga na kuongoza filamu ya vichekesho ya Der die Tollkirsche ausgräbt (filamu ya kimya-kimya).
Maisha binafsi
[hariri | hariri chanzo]Pale anasimama kufanya kazi zake, basi huwa na kawaida ya kuishi mjini Berlin. Alisha wahi kutembea na mwigizaji filamu wa Kimarekani, Elijah Wood na mwongozaji filamu Tom Tykwer. Mnamo mwaka wa 2008, amevishwa pete na mfanya biashara wa Kimarekani. Alishawahi kusema kuwa mchumba wake anaitwa Dio na hivyo wana mpango wa kuwa na watoto.[5]
Filamu
[hariri | hariri chanzo]Mwaka | Filamu | Jina alilotumia | Maelezo mengine |
---|---|---|---|
1995 | It's a Jungle Out There | Anna | Tuzo za Filamu za Bavaria - Mwigizaji Bora |
1997 | Coming In | Nina | Filamu ya Televisheni |
1998 | Opernball | Gabrielle Becker | Televisheni filamu Bavarian TV Award - Mwigizaji Bora |
Run Lola Run | Lola | Bambi Award - Mwigizaji Bora | |
Bin ich schön? | Linda | ||
2000 | Anatomy | Paula Henning | |
The Princess and the Warrior | Simone 'Sissi' Schmidt | ||
2001 | Blow | Barbara Buckley | |
Storytelling | Editor | ||
2002 | The Bourne Identity | Marie Helena Kreutz | |
All I Want | Jane | ||
2003 | I Love Your Work | Mia | |
Blueprint | Iris Sellin/Siri Sellin | ||
2004 | The Bourne Supremacy | Marie Helena Kreutz | |
Creep | Kate | ||
2005 | The Elementary Particles | Annabelle | |
2006 | The Shield | Diro Kesakhian | |
2007 | Romulus, My Father | Christine Anna Gaita (née Dörr) | |
2007 | The Bourne Ultimatum | Marie Helena Kreutz | Vipande vya awali |
2008 | Guerrilla | Tamara Bunke | |
The Argentine | Tamara Bunke | ||
La traque – Die Hetzjagd | Beate Klarsfeld | Televisheni filamu | |
2008 | Die Brücke | Elfie Bauer | Televisheni filam; marudio ya filamu ya Bernhard Wicki' Die Brücke (1959) |
2009 | Shanghai | TBA | Marudio ya filamu ya [Shanghai (1935) |
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Mahojiano na Marie Claire (2002) Archived 18 Julai 2011 at the Wayback Machine.(Ujerumani)
- ↑ "Franka Potente". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2010-08-21. Iliwekwa mnamo 2008-12-04.
- ↑ Wasifu wa Franka Potente (1974-)
- ↑ [1]Berliner Morgenpost, 3/6/2005 (German)
- ↑ http://www.bild.de/BILD/unterhaltung/leute/2008/08/06/franka-potente/mit-us-amerikaner-verlobt-wuenscht-sich-kinder.html