Nenda kwa yaliyomo

Francesca Gargallo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Francesca Gargallo (25 Novemba 1956 – 3 Machi 2022) alikuwa mwandishi na mshairi wa Meksiko aliyezaliwa Sicilia.

Maisha na kazi

[hariri | hariri chanzo]

Alizaliwa Siracusa, Italia kwa jina Francesca Gargallo di Castel Lentini Celentani. Alisomea falsafa katika Chuo Kikuu cha Roma (Università degli studi di Roma) na baadaye katika Chuo Kikuu cha Kitaifa cha Uhuru cha Meksiko (UNAM).

Alipata uraia wa Meksiko na aliishi nchini humo tangu mwaka 1979. Aliandika vitabu vingi vya mashairi na riwaya kama vile Calla mi amor que vivo, Estar en el mundo, La decisión del capitán, na Marcha seca, miongoni mwa vingine.[1]

Gargallo pia alichapisha kazi zake katika majarida mbalimbali kama vile Proceso.

Alifariki kutokana na saratani tarehe 3 Machi 2022 akiwa na umri wa miaka 65.[2]

  1. ["Red) mundial de escritores en Español - Francesca Gargallo". {{cite web}}: Check |url= value (help)
  2. ["La) Jornada - Fallece Francesca Gargallo, escritora, activista y docente de la UNAM". [www.jornada.com.mx](http://www.jornada.com.mx). {{cite web}}: Check |url= value (help)
Makala hii kuhusu mwandishi fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Francesca Gargallo kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.