Nenda kwa yaliyomo

Fouzia Rhissassi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Fouzia Rhissassi (alizaliwa 1947) ni msomi, mwandishi, na mwanaharakati wa haki za wanawake kutoka nchini Moroko.

Anajulikana kimataifa kwa mchango wake katika kukuza masomo ya kijinsia (gender studies) katika vyuo vikuu vya Moroko na kwa kazi yake kama mshauri katika masuala ya elimu na haki za binadamu[1].

Fouzia Rhissassi alizaliwa tarehe 15 Aprili 1947 katika mji wa Fes, nchini Morocco.

Rhissassi amekuwa akifundisha tangu mwaka 1974. Katika kipindi cha taaluma yake, alisimamia tasnifu nyingi za shahada ya kwanza, uzamili na uzamivu.

Kupitia kazi zake katika Masomo ya Wanawake na masuala ya Amani katika ulimwengu wa Kiarabu, Profesa Rhissassi ameandika machapisho mengi. Amekuwa mhariri wa mradi wa UNESCO uitwao “The Woman and Her Rights” pamoja na Abderrazak Moulayrohid mwaka 2004, na pia ameandika kuhusu waandishi wanawake wa Morocco wanaotumia lugha ya Kiarabu.

Aidha, amechangia katika uwanja wa Masomo ya kijinsia kupitia kazi kama “dhana kuu za elimu, maadili na michakato ya kuhakikisha jamii endelevu; mfano wa Morocco”. Mbali na kuandika machapisho mengi, pia ameshiriki katika matukio mbalimbali kama mhadhiri au mjumbe kulingana na utaalamu wake.[2]

Tuzo na heshima

[hariri | hariri chanzo]
  • Tuzo ya mwaka 2006 katika kundi la haki za binadamu (tuzo hii hutolewa kila mwaka kwa wanawake mashuhuri wa Morocco kwa mafanikio yao).[3]
  • Nishani ya Wissam of the Alouite Throne, mwaka 1993.[4]
  • Cheo cha chevalier de l’ordre de la Couronne kilichotolewa na Mfalme Albert II of Belgium mwaka 2004 nchini Belgium.[4]
  • Tuzo ya Gold Leaf kutoka ubalozi wa Canada nchini Morocco mwaka 2007.[4]
  1. Fernea, Elizabeth Warnock (1998). In search of Islamic feminism: one woman's global journey (tol. la 1st ed). New York: Doubleday. ISBN 978-0-385-47518-1. {{cite book}}: |edition= has extra text (help)
  2. Al-Raida, Beirut University College. Institute for Women's Studies in the Arab World, ed. The Institute, 2003, uk. 37
  3. "Lesieur Cristal" (kwa Kifaransa). Lesieur-cristal.ma. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-03-04. Iliwekwa mnamo 2015-02-28.
  4. 1 2 3 "Femmes, droit de la famille et systeme judiciaire en Algerie, au Maroc et en Tunisie" (PDF). Unesdoc.unesco.org. Iliwekwa mnamo 2015-02-28.
Makala hii kuhusu mwandishi fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Fouzia Rhissassi kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.