Flurazepam
| Jina la (IUPAC) | |
|---|---|
| 7-Chloro-1-[2-(diethylamino)ethyl]-5-(2-fluorophenyl)-1,3-dihydro-2H-1,4-benzodiazepin-2-one | |
| Data ya kikliniki | |
| Majina ya kibiashara | Dalmane, Dalmadorm, Fluzepam, mengineyo |
| AHFS/Drugs.com | Monograph |
| MedlinePlus | a682051 |
| Kategoria ya ujauzito | X (Haishauriwi kutumika) |
| Hali ya kisheria | ? (CA) ? (US) |
| Njia mbalimbali za matumizi | Kwa mdomo |
| Data ya utendakazi | |
| Uingiaji katika mzunguko wa mwili | 83% |
| Kimetaboliki | Ini |
| Nusu uhai | Masaa 2.3 N-desalkylflurazepam: Masaa 47–100 |
| Utoaji wa uchafu | Figo |
| Vitambulisho | |
| Nambari ya ATC | ? |
| Visawe | Flurazepam hydrochloride |
| Data ya kikemikali | |
| Fomyula | C21H23ClFN3O |
| |
| Data ya kimwili | |
| Kiwango cha kuyeyuka | 79.5 °C (175 °F) |
| | |
Flurazepam, inayouzwa kwa jina la chapa ya Dalmane miongoni mwa mengine, ni dawa inayotumika kutibu matatizo ya kulala.[1] Inaweza kuwa muhimu kwa hadi wiki nne.[2] Dawa hii inachukuliwa kwa mdomo [1] na athari yake huanza ndani ya dakika 45 na hudumu hadi masaa manane.[2]
Madhara yake ya kawaida ni pamoja na kizunguzungu, uratibu duni na kuanguka chini.[2] Madhara yake mengine yanaweza kujumuisha uraibu, kujiua na msisimko.[2] Matumizi yake na afyuni kwa ujumla hayapendekezwi.[2] Matumizi yake wakati wa ujauzito yanaweza kumdhuru mtoto.[2] Dawa hii ni ya kundi la benzodiazepine.[2]
Flurazepam ilipewa hati miliki na ikaanza kutumika katika matibabu mwaka wa 1968.[3] Nchini Uingereza, vidonge 30 iligharimu Huduma ya Kitaifa ya Afya (NHS) chini ya £10 kufikia mwaka wa 2021.[1] Kiasi hiki nchini Marekani ni takriban dola 16.[4]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- 1 2 3 BNF 81: March-September 2021. BMJ Group and the Pharmaceutical Press. 2021. uk. 508. ISBN 978-0857114105.
- 1 2 3 4 5 6 7 "Flurazepam Monograph for Professionals". Drugs.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 6 Mei 2021. Iliwekwa mnamo 14 Desemba 2021.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Fischer, Jnos; Ganellin, C. Robin (2006). Analogue-based Drug Discovery (kwa Kiingereza). John Wiley & Sons. uk. 538. ISBN 9783527607495. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-11-01. Iliwekwa mnamo 2021-10-22.
- ↑ "Flurazepam Prices, Coupons & Savings Tips - GoodRx". GoodRx. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 12 Oktoba 2016. Iliwekwa mnamo 14 Desemba 2021.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)