Floriani wa Lorch

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta

Floriani wa Lorch (alifia dini tarehe 4 Mei 304) alikuwa askari Mkristo wa Dola la Roma aliyeishi Mantem, karibu na Kirchdorf an der Krems, leo nchini Austria.

Aliposikia kwamba Akwilino, wakati wa dhuluma ya kaisari Dioclesyano, amekamata Wakristo 40 mjini Lorch, alitamani kuwa nao akaenda huko. Karibu na kufika alikutana na askari wenzake akajitambulisha kuwa Mkristo, hivyo akakamatwa na kupelekwa kwa Akwilino. Huyo alijaribu kumfanya atoe sadaka kwa miungu, lakini alipokataa aliagoza apigwe mijeledi na kutupwa katika mto Enns akiwa na jiwe kubwa limefungwa shingoni.

Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu mfiadini.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifo chake.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Christian cross.svg Makala hii kuhusu Mkristo huyu bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Floriani wa Lorch kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.