Nenda kwa yaliyomo

Flora Sandes

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Flora Sandes akiwa amevaa mavazi ya kijeshi

Flora Sandes (Kiserbia Флора Сендс, Januari 1876 - Novemba 1956) ni mwanamke mwingereza aliyehudumu kama mwanachama wa jeshi la kifalme la Serbia katika Vita vya Kwanza vya Dunia. Alikuwa mwanamke pekee kutoka Uingereza aliyeruhusiwa rasmi kuhudumu kama mwanajeshi katika vita hivyo.[1] Hapo awali, alikuwa mfanyakazi wa kujitolea wa huduma ya ambulansi ya Mt. Yohana, alisafiri hadi Ufalme wa Serbia, ambako alikaribishwa na kusajiliwa rasmi katika jeshi la Serbia. Baadaye alipandishwa cheo hadi kuwa Meja sajenti, na baada ya vita alipandishwa tena hadi cheo cha Kapteni Mwandamizi. Alitunikiwa medali saba.

Flora Sandes alizaliwa mnamo Januari 1876 huko Nether Poppleton, Yorkshire, akiwa mtoto wa mwisho wa kike katika familia ya asili  ya Eire. Baba yake alikuwa Samuel Dickson Sandes (18221914), aliyekuwa mkuu wa Whitchurch, Kaunti ya Cork, na mama yake alikuwa Sophia Julia.[2][3] Alipokuwa na umri wa miaka tisa, familia yao ilihamia kijiji cha Marlesford, Suffolk na baadaye eneo la Thornton Heath, karibu na mji wa Croydon, Surrey.[2] Akiwa mtoto alielimishwa nyumbani na walimu wa binafsi.[3] Alipenda kupanda farasi na kutumia bunduki na aliwahi  kusema kwamba alitamani angezaliwa mvulana.[4] Alijifunza kuendesha gari na kuendesha gari la zamani la mashindano la kutoka Ufaransa.[4] Baadae alipata kazi ya ukatibu.[4]

Sandes alijiunga na kitengo cha Ambulensi cha Mtume Yohana kilicholelewa na muuguzi kutoka Marekani anayeitwa Mabel Grouitch, na mnamo Agosti 1914 aliondoka Uingereza kwenda Serbia akiwa na kundi la wanawake jumla ya 36 kwa ajili ya kusaidia migogoro ya kibinadamu.[2][4][5] Walifika katika mji wa Kragujevac, ambao ulikuwa kituo cha vikosi vya Serbia vilivyopigana dhidi ya mashambulizi ya Austria-Hungaria. Sandes alijiunga na Msalaba Mwekundu wa Serbia na kufanya kazi katika gari la wagonjwa kwa ajili ya kikosi cha pili cha askari wa miguu cha Jeshi la Serbia.[2] Mnamo mwaka 1914, alipanda farasi pamoja na askari wa Serbia ambaye, alivutiwa na ujuzi wake wa kupanda farasi, alimwambia kwamba alikuwa amepoteza muda kama muuguzi na anapaswa kujiandikisha kama mwanajeshi; Sandes alimwambia Dkt. Isabel Emslie, "Siku zote nimetamani kuwa mwanajeshi na kupigana."

Baadaye Sandes alirudi Uingereza. Alitumia miaka yake ya mwisho huko Suffolk, akiishi katika Kijiji cha Hacheston karibu na Soko la Wickham. Alifariki mashariki mwa Suffolk katika hospitali ya Ipswich mnamo Novemba 1956.[3] Alichomwa moto katika Kituo cha maiti cha Ipswich na majivu yake yakatawanywa katika bustani ya ukumbusho. Katika Kanisa la Mt.Andrea lililopo Marlesford, kuna bamba la kumbukumbu lililowekwa kwa heshima yake kwenye ukuta wa kusini katika viti vya kwaya.

  1. "A forgotten soldier on a forgotten front". www.bbc.co.uk (kwa Kiingereza (Uingereza)). Iliwekwa mnamo 2026-01-29.
  2. 1 2 3 4 Hartley, Cathy (2003). A Historical Dictionary of British Women (kwa Kiingereza). Psychology Press. ISBN 978-1-85743-228-2.
  3. 1 2 3 "Dictionary of National Biography", Wikipedia (kwa Kiingereza), 2026-01-20, iliwekwa mnamo 2026-01-29
  4. 1 2 3 4 Hazen, Walter A. (2006). World War I (kwa Kiingereza). Good Year Books. ISBN 978-1-59647-074-3.
  5. Jones, David E. (2000). Women Warriors: A History (kwa Kiingereza). Potomac Books, Incorporated. ISBN 978-1-57488-206-3.
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Flora Sandes kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.