Fina Girard
Fina Girard alizaliwa Oktoba 20 2001, ni mwanaharakati wa masuala ya hali ya hewa na mwanasiasa kutoka nchini uswizi ambaye amehudumu katika baraza kuu la Basel-Stadt tangu 2023. Pia ni wanachama wa Green Party na Young Greens, aliwakilisha Grossbasel-west constituency. Kabla ya kuingia kwenye siasa, alikuwa mwanachama wa mgomo wa hali ya hewa wa Basel na alikuwa rais-mwenza wa tawi la Young Greens.
Wasifu
[hariri | hariri chanzo]Maisha ya awali na Uharakati:
[hariri | hariri chanzo]Fina Girard alizaliwa tarehe 20 Oktoba 2001 katika mji wa Basel, Uswizi.[1]Akiwa binti wa dereva teksi na msimamizi wa makumbusho, alisoma kaitaka shule ya Gymnasium Leonhard. Akiwa na umri wa miaka kumi na minne(14) alijiungana kikundi cha vijana Amnesty International katika mji wa Basel, na akamaliza mwaka mzima wa mafunzo ya vitendo akiwa na Amnesty International baada ya kuhitimu elimu ya sekondari.[2][3] Girard anasoma sayansi ya siasa na jiografia kaitka chuo kikuu cha Besel.[4]
Girard amekuwa akishiriki kikamilifu katika mgomo wahali ya hewa wa Basel tangu mwaka 2019, na alijiunga na Young Green Alliance Northwest tawi la enea hilo la Young Greens mwaka unaofuata.Katika uchaguzi wa 2020 kwa ajili ya Grand Council of Basel-Stadt, Girard aligombea kama mgombea wa chama cha Green Party, lakini alishindwa vibaya.Mnamo mwezi Agosti 2021, alichaguliwa kuwa raisi mwenza wa Young Green Alliance Northwest, nahapo awali alikuwa mwanachama wa bodi yake.[5][6]Pia, yeye ni mwanachama aliyachaguliwa na Alliance F.[7]
Kazi ya siasa
[hariri | hariri chanzo]Mnamo tarehe 8 Februari 2023, Girard aliteuliwa katika baraza kuu la Basel-Stadt kuchukuwa nafasi ya Beatrice Messerali, ambaye alijiuzulu.Anawakilisha jimbo la Grossbasel-West kama mwanachama wa Green-Alternative Alliance, na anahudumu katika tume ya uchumi na kodi, tume ya nidhamu, na Tume ya Msamaha.Wakati wa kuteuliwa kwake,Girard alikuwa mmoja wa wanachama wanne wa Young Greens waliohudumu katika Baraza Kuu.[1][4]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- 1 2 "Frau Fina Girard". Grosser Rat des Kantons Basel-Stadt (kwa Kijerumani). Iliwekwa mnamo 2025-10-13.
- ↑ Rohner, Isabel; Schäppi, Irène (2020-11-20). 50 Jahre Frauenstimmrecht: 25 Frauen über Demokratie, Macht und Gleichberechtigung (kwa Kijerumani). Limmat Verlag. ISBN 978-3-03855-218-5.
- ↑ "Fina Girard, 18 ans, une recherche de sens". Amnesty International Suisse (kwa Kifaransa). Iliwekwa mnamo 2025-10-13.
- 1 2 "Web-Mitteilungen". Grosser Rat des Kantons Basel-Stadt (kwa Kijerumani). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2025-05-28. Iliwekwa mnamo 2025-10-13.
- ↑ "Klimakrise: Warum wir uns selbst am nächsten sind". ellexx (kwa Kijerumani). 2021-11-15. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2025-11-07. Iliwekwa mnamo 2025-10-13.
- ↑ Ahmeti, Ali, "Basel: Junges Grünes Bündnis wählt neues Co-Präsidium", Luzerner Zeitung (kwa Swiss High German), iliwekwa mnamo 2025-10-13
- ↑ "Nordwestschweiz". alliance F (kwa Swiss High German). Iliwekwa mnamo 2025-10-13.