Livingstone (filamu)
Mandhari
(Elekezwa kutoka Filamu ya Livingstone)
Livingstone ni filamu ya kimya ya Kizungu iliyotengenezwa mwaka 1925, ambayo iliandaliwa na kuongozwa na kuchezwa na M.A.Wetherell kama muhusika mkuu. Pia imewashirikisha Molly Rogers na Henry Walton. Filamu hii inaonyesha maisha ya David Livingstone, anayejulikana kama Bula Matari, ambaye alikua mmisionari wa Uskoti akijitahidi kukomesha utumwa na kuleta elimu Afrika pia inaonyesha tukio lake maarufu la kukutana na Henry Morton Stanley.