Nenda kwa yaliyomo

Fettouma Touati

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Fettouma Touati (alizaliwa mnamo mwaka 1950) ni mwandishi wa riwaya mwenye asili ya Algeria na Ufaransa, na huandika kwa lugha ya Kifaransa.[1]

Fettouma Touati alizaliwa Azazga, kijiji kidogo cha milimani katika eneo la Kabylia nchini Algeria. Wazazi wake walihamia Ufaransa mwaka 1951, kabla ya Vita vya Uhuru wa Algeria. Mwaka 1975, alirudi Kabylia kwa kipindi cha miaka minne, ambapo alifanya kazi kama mtunza maktaba katika Chuo Kikuu cha Tizi Ouzou.[2]

Riwaya yake Le printemps désespéré inaeleza maisha ya vizazi vitatu vya wanawake wa Algeria, ikionyesha jinsi mtandao wa mahusiano ya wanawake ulivyowasaidia kukabiliana na ubaguzi wa rangi na wa kijinsia waliokuwa wakikumbana nao mara kwa mara.[3][4]

  • Le printemps désespéré: vies d'Algériennes. 1984. Imetafsiriwa kwa lugha ya kiingereza na Ros Schwartz ikipewa jina la : Desperate Spring, he Women's Press, mnamo mwaka 1987.[5]
  1. Moore, Lindsey (2008-05-14). Arab, Muslim, Woman: Voice and Vision in Postcolonial Literature and Film (kwa Kiingereza). Routledge. ISBN 978-1-134-13878-4.
  2. "Desperate Spring". The Arab British Centre (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2026-03-27.
  3. "Desperate Spring: Lives of Algerian Women". AfricaBib (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2026-03-27.
  4. "Student Encyclopedia of African Literature". EPDF (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2026-03-27.
  5. "Le printemps désespéré : vies d'algériens". Librairies Boyer (kwa Kifaransa). Iliwekwa mnamo 2026-03-27.
Makala hii kuhusu mwandishi fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Fettouma Touati kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.