Nenda kwa yaliyomo

Fernande Decruck

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Fernande Decruck (née Breilh; 25 Desemba 1896 – 6 Agosti 1954) alikuwa mtunzi wa muziki wa Ufaransa aliyebobea hasa katika utunzi wa kazi za saxofoni, akiwa ametunga zaidi ya kazi 40 kwa ala hiyo. Kazi yake inayojulikana zaidi ni *Sonata katika C♯ minor* kwa saxofoni ya alto au viola, iliyotolewa kwa Marcel Mule.

Fernande Breilh alizaliwa katika kijiji cha Gaillac, Ufaransa, katika familia ya mfanyabiashara wa eneo hilo. Alianza kujifunza piano akiwa na umri wa miaka nane na baadaye alisoma katika Konsevatori ya Toulouse.

Mwaka 1918 alikubaliwa katika Konsevatori ya Paris akisoma ogani na utunzi wa muziki. Akiwa huko, alishinda tuzo katika masomo ya harmonia, fuga, kontrapointi na uambatanishaji wa piano.

Makala hii kuhusu mwanamuziki fulani wa Ulaya bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Fernande Decruck kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.