Nenda kwa yaliyomo

Fernão do Pó

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Fernão do Pó (pia anajulikana kama Fernão Pó, Fernando Pó au Fernando Poo; aliishi karne ya 15) alikuwa baharia na mchunguzi kutoka Ureno katika karne ya 15 aliyechunguza pwani ya Afrika Magharibi. Alikuwa Mzungu wa kwanza kuona visiwa vilivyoko katika Ghuba ya Guinea takribani mwaka 1472.

Kisiwa kimojawapo, kilichobeba jina lake hadi katikati ya karne ya 20, kilijulikana kama Fernando Pó au Fernando Poo. Sasa kisiwa hicho kinaitwa Bioko na ni sehemu ya Guinea ya Ikweta. Jina lake pia limepewa maeneo mengine kadhaa, ikiwemo kijiji cha Fernando Pó huko Ureno na kijiji cha Fernando Pó huko Sierra Leone.[1]

  1. Liniger-Goumaz, Max. 1979. Historical dictionary of Equatorial Guinea. Metuchen, N.J. (USA): Scarecrow Press. ISBN 0-8108-1230-4.
    • Room, Adrian. 1994. African placenames. Jefferson, N.C. (USA): McFarland. ISBN 0-89950-943-6
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Fernão do Pó kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.