Felix A. Chami
Mandhari
Felix A. Chami ni mtaalamu wa akiolojia kutoka Tanzania. Yeye ni profesa katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, akijikita katika akiolojia ya pwani ya Afrika Mashariki. Dr. Chami aligundua, katika visiwa vya Mafia na Juani, mabaki ya kihistoria yaliyofichua kwamba Afrika Mashariki ilikuwa sehemu muhimu ya biashara ya Bahari ya Hindi.
Chami alipata shahada yake ya kwanza ya sosholojia katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka 1986, shahada ya uzamili ya anthropolojia katika Chuo Kikuu cha Brown mwaka 1988, na shahada ya uzamivu (Ph.D.) ya akiolojia katika Chuo Kikuu cha Uppsala mwaka 1994.[1]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]| Makala hii kuhusu wasifu wa Mtanzania bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |