29 Februari

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Februari 29)
Jan - Februari - Mac
1 2 3 4 5 6 7
8 9 10 11 12 13 14
15 16 17 18 19 20 21
22 23 24 25 26 27 28
29
Kalenda ya Gregori

29 Februari ni siku ya pekee katika kalenda kwa sababu haipo kila mwaka. Inaweza kutokea baada ya miaka minne pekee lakini kwa utaratibu maalum. Kuwepo kwa tarehe hiyo kunafanya mwaka kuwa mwaka mrefu wa siku 366.

Utaratibu wa kupatikana kwa 29 Februari[hariri | hariri chanzo]

Inatokea tu kila mwaka wa nne kama namba ya mwaka inagawika kwa 4 kama vile 2004, 2008, 2012, 2016, 2020, 2024, 2028. Lakini haipo tena katika kila mwaka ambao namba yake hugawika kwa 100 kama vile miaka 1800, 1900, 2100 isipokuwa ipo tena katika miaka ambayo namba hugawika kwa 400 kama vile 1600, 2000, 2400, 2800.

Ikiwepo ni siku ya sitini ya mwaka. Mpaka uishe zinabaki siku 306.

Sababu ya kuwepo kwa 29 Februari[hariri | hariri chanzo]

29 Februari kama siku ya nyongeza inaingizwa katika kalenda ya kawaida ili kuratibu urefu wa mwaka wa kalenda na majira yaani na mwendo wa Dunia ukizunguka Jua kwenye obiti yake.

Kalenda hutumia kizio cha siku, yaani muda wa Dunia kuzunguka kwenye mhimili wake, kuanzia machweo ya Jua hadi machweo yanayofuata. Katika muda wa mwaka 1 kuna siku zaidi ya 365; kwa wastani mwaka huwa na sekunde 31,536,000 au siku 365.2425 yaani karibu siku 365 na robo lakini kidogo chini yake. Tofauti hiyo ya karibu robo siku husawazishwa kwa kuingiza siku ya nyongeza kila baada ya miaka minne lakini kuipumzisha mara tatu kila baada ya miaka 100, ikirudiwa kila baada ya miaka 400.

Bila kuwepo kwa siku ya nyongeza majira na mwendo wa Jua yangeachana, hali inayoonekana zaidi kwenye sehemu za Dunia zisizo karibu na ikweta. Hali hiyo ilitokea tayari hadi matengenezo ya kalenda katika karne ya 17 yaliyoleta Kalenda ya Gregori.

Matukio[hariri | hariri chanzo]

Waliozaliwa[hariri | hariri chanzo]

Waliofariki[hariri | hariri chanzo]

Sikukuu[hariri | hariri chanzo]

Wakristo wengi, wakifuata mapokeo ya Roma, huadhimisha kumbukumbu za watakatifu Papa Hilarius, Oswadi wa York, Augusto Chapdelaine n.k.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu 29 Februari kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.