Fausto wa Milevi
Mandhari
Fausto wa Milevi alikuwa askofu wa Umani wa karne ya 4. Anakumbukwa kwa kukutana kwake na Agostino wa Hippo, huko Karthago yapata mwaka 383. Alitokea Milevi, Numidia (Aljeria ya sasa). Kutoka katika malezi maskini ya kipagani, alipata kuwa mwalimu, mhubiri na mtu wa majadiliano mwenye sifa nzuri.