Nenda kwa yaliyomo

Fausta wa Kuziko

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mchoro mdogo wa kifodini chake pamoja na Evilasius na Masimo.

Fausta wa Kuziko (alifariki 311) alikuwa msichana mwenye umri wa miaka 13 ambaye alishuhudia kwa ujasiri imani yake ya Kikristo, hata akamfanya kuhani Mpagani Evilasius aliyemtesa abadilike na kuwa Mkristo kama yeye, hatua iliyokuwa na adhabu ya kifo katika mji wa Kuziko, kwa kuwa wakazi wake hawakutaka mtu yeyote kubadili dini tofauti na imani yao ya wakati huo[1].

Tangu kale wote wawili wanahesabika miongoni mwa watakatifu wafiadini[2], pamoja na hakimu Masimo aliyeagiza wauawe akajiunga nao.

Sikukuu yao huadhimishwa na Wakatoliki tarehe 20 Septemba[3], ila kwa Waorthodoksi tarehe 5 Februari.

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
  1. https://www.santiebeati.it/dettaglio/100178
  2. Catholic Online
  3. https://www.santiebeati.it/dettaglio/70900
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.