Fatou Bensouda

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Fatou Bensouda mnamo 2008

Fatou Bom Bensouda (* Banjul, 31 Januari 1961) ni mwanasheria kutoka nchini Gambia. Alikuwa Waziri wa Sheria wa Gambia na tangu mwaka 2012 ni mwendesha mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai.

Bensouda alisoma sheria nchini Nigeria na sheria za bahari nchini Malta.  Baada ya uasi wa kijeshi nchini Gambia wa mwaka 1994 rais mpya Yahya Jammeh alimchukua Bensouda kuwa mshauri wake wa kisheria. Kuanzia mwaka 1998 hadi 2000 alikuwa Waziri wa Sheria wa Gambia.

Mwaka 2000 alihamia Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ya Rwanda huko Arusha (Tanzania) kama mwendesha mashitaka. Kazi alifanya kuanzia mwaka 2002 hadi Agosti 2004.

Kutoka hapo aliendelea kwenda Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) mjini Den Haag (Uholanzi). Katika Septemba 2004, alikuwa naibu mwendesha mashtaka na akawapa uongozi wa ofisi ya mwendesha mashitaka, Luis Moreno-Ocampo.

Bensouda ameolewa na mfanyabiashara na ni mama wa watoto watatu.