Fatimatu Abubakar
Fatimatu Abubakar ni mwanasheria, mwanasiasa na mjasiriamali wa Ghana. Yeye ni mwanachama wa New Patriotic Party na kwa sasa ni Waziri wa Habari.
Kabla ya kuwa Waziri, Fatimatu aliwahi kuwa Naibu Waziri wa Habari na pia Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano katika Ofisi ya Rais. Kabla ya kazi zake za kisiasa, aliwahi kufanya kazi Lansdown Resort, Aburi kama msimamizi wa nyumba, na SRM Engineering Limited kama afisa wa ofisi (Clerk). Fatimatu alisoma Saikolojia na lugha ya Kiingereza katika shahada yake ya kwanza na ya pili.
Fatimatu Abubakar aliteuliwa kuwa Waziri mpya wa Habari tarehe 14 Februari 2024, akichukua nafasi kutoka kwa Kojo Oppong Nkrumah.[1][2][3][4][5]
Maisha ya awali na elimu
[hariri | hariri chanzo]Fatimatu alizaliwa Kumasi, katika Mkoa wa Ashanti. Alipata shahada ya kwanza katika Saikolojia na Lugha ya Kiingereza kutoka Chuo Kikuu cha Ghana.
Mwaka 2008, akiwa chuoni, aliwahi kuwa Makamu wa Rais wa Akuafo Hall Junior Common Room, na mwaka 2010 alishindania nafasi ya Katibu Mtendaji wa Umoja wa Wanafunzi Kitaifa wa Ghana (NUGS).
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Akufo-Addo swears-in 24 new ministers and deputy ministers". Citinewsroom - Comprehensive News in Ghana (kwa American English). 2024-05-21. Iliwekwa mnamo 2024-06-12.
- ↑ "Fatimatu Abubakar – Ministry Of Information Ghana". moi.gov.gh. Iliwekwa mnamo 2024-06-12.
- ↑ "Fatimatu Abubakar – Ministry Of Information Ghana". moi.gov.gh. Iliwekwa mnamo 2024-06-12.
- ↑ "Fatimatu Abubakar – Ministry Of Information Ghana". moi.gov.gh. Iliwekwa mnamo 2024-06-12.
- ↑ "Fatimatu Abubakar – Ministry Of Information Ghana". moi.gov.gh. Iliwekwa mnamo 2024-06-12.
| Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Fatimatu Abubakar kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |