Nenda kwa yaliyomo

Fatima Zohra Ardjoune

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Fatima Zohra Ardjoune ni jenerali wa Jeshi la nchi ya Algeria. Yeye ndiye mwanamke wa kwanza katika ulimwengu wa Kiarabu kufikia cheo hiki. Pia kiwa daktari, alianzisha utafiti katika uwanja wa hematolojia nchini humo katika miaka ya 1980. Anahudumu kama mkurugenzi mkuu wa hospitali kuu ya kijeshi.

Maisha ya Awali na Taaluma

[hariri | hariri chanzo]

Fatima Zohra Ardjoune alizaliwa katika mji wa Sétif na alipata Elimu ya msingi katika shule ya indigenous primary school iliyofuatiwa na shule ya sekondari ya juu ya wasichana mjini Kouba. Kama mtoto alitamani kusaidia wengine na alienda kusomea udaktari katika chuo kikuu cha Algiers[1]

  1. Kechar, Mounir (31 March 2014). "Pr Fatima Zohra Ardjoune, la première femme général de l'armée algérienne" (in French). Algeria Blanche. Retrieved 17 April 2018.