Fatima Waziri-Azi
| Fatima Waziri–Azi | |
Director General, NAPTIP | |
| Aliingia ofisini 8 September 2021 | |
| mtangulizi | Senator Basheer Garba Muhammed |
|---|---|
Former Head of Department of Public Law at the Nigerian Institute of Advanced Legal Studies | |
| mhitimu wa | Ahmadu Bello University, Zaria Havard Business School, University of Pittsburgh |
| taaluma | Lawyer |
Fatima Waziri-Azi ni wakili wa kutoka Nchini Nigeria na pia ni Mkurugenzi Mkuu katika Shirika la Kitaifa llinalohusika na Kupiga Marufuku Usafirishaji Haramu wa Watu (NAPTIP) la nchini Nigeria. . Kabla ya kuteuliwa kwake NAPTIP alikuwa mshauri wa utawala wa sheria wa Rais wa Nigeria, aliyeitwa Muhammadu Buhari . Yeye ni Mkuu wa zamani wa Idara ya Sheria ya Umma katika Taasisi ya Mafunzo ya Kisheria ya Juu ya Nigeria [1] na yeye ni mtetezi wa haki za wanawake na mwanaharakati dhidi ya unyanyasaji wa majumbani na kingono.
Elimu
[hariri | hariri chanzo]Fatima Waziri-Azi alisoma katika Chuo Kikuu cha Ahmadu Bello, Zaria, na kupata shahada ya kwanza katika Sheria mnamo mwaka wa 2001. [2] Yeye ni Mwanachama Mshiriki katika Taasisi ya Wasuluhishi ya nchini Uingereza; na ni mwanachama wa Chama cha Wanasheria cha nchini Nigeria, Chama cha Wanasheria cha Kaunti ya New York, Chama cha Wanawake katika Maendeleo na cha Wanawake katika Usalama wa Kimataifa .
Kazi
[hariri | hariri chanzo]Tangu Januari mwaka wa 2005 hadi Agosti Agosti mwaka wa 2006, Fatima Waziri-Azi alifanya kazi kama wakili au afisa mwandamizi wa programu katika Dawati la Haki za Wanawake, Masuala ya Uchaguzi, na Mageuzi ya Sekta ya Haki. [3] Kuanzia mwezi Februari mwaka wa 2016 hadi mwezi Novemba mwaka wa 2018, alifanya kazi kama afisa wa utafiti na programu katika Kamati ya Ushauri ya Rais Dhidi ya Rushwa (PACAC). Kuanzia mwezi Novemba mwaka wa 2018, alifanya kazi kama Mshauri wa Utawala wa Sheria kwa Rais katika Ofisi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Shirikisho la Nigeria. Mnamo mwezi Septemba na mwaka wa 2021, Fatima Waziri-Azi aliteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kitaifa la Kupiga Marufuku Usafirishaji Haramu wa Binadamu (NAPTIP) . [4]
Tuzo
[hariri | hariri chanzo]- Tuzo ya Kimataifa ya Mafanikio ya Vijana wa Sheth [5]
- Crouch - Kielsgard Scholarship ya Programu ya Haki za Kibinadamu ya Tamaduni Mbalimbali (ya mwaka wa 2006)
- Tuzo la Insha la Siegfried Wiessner (ya mwaka wa 2007)
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Meet Fatima Waziri-Azi: New Director General Of NAPTIP | The Abusites" (kwa American English). 2021-09-10. Iliwekwa mnamo 2022-03-29.
- ↑ Admin (10 Septemba 2021). "Meet Fatima Waziri-Azi: New Director General of NAPTIP | the Abusites".
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Ambali, Fehintola (2021-09-13). "Amazing CV Of NAPTIP DG Waziri-Azi" (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2022-03-30.
- ↑ "Fatima Waziri-Azi: NAPTIP new Director General wey President Buhari appoint - Profile". BBC News Pidgin. 9 Septemba 2021. Iliwekwa mnamo 30 Machi 2022.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Dr. Fatima Waziri-Azi (JD '11) Receives Sheth International Young Alumni Achievement Award | School of Law". www.law.pitt.edu. Iliwekwa mnamo 2025-04-07.