Nenda kwa yaliyomo

Fatima Batul Mukhtar

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Fatima Batul Mukhtar

Prof Fatima Batul Muktar picture


mtangulizi Professor Jibrilla Dahiru Amin
aliyemfuata Professor Abdulkarim Sabo Muhammad

aliyemfuata Professor Isyaku Ibrahim Indabawa

aliyemfuata Professor Amina Salihi Bayero

Tarehe ya kuzaliwa 23 Mei 1963 (1963-05-23) (umri 63)
Kano
Mahusiano Married
Mhitimu wa Bayero University, Kano
Ahmadu Bello University, Zaria
Fani yake Academic

Fatima Batul Mukhtar (alizaliwa Mei 23, 1963) ni msomi mwanamke anayefanya kazi kama profesa wa mimea kutoka nchi ya Nigeria ambaye mwenye kushika nafasi ya makamu mkuu wa Chuo Kikuu cha Azman Kano. Maeneo yake ya utafiti yanajikita juu ya udhibiti wa ukuaji, takwimu za kibiolojia, teknolojia ya mimea na utunzaji wa mimea. Alichaguliwa nafasi ya makamu mkuu wa Chuo Kikuu cha Shirikisho cha Dutse na Rais Muhammadu Buhari na ameshika nafasi hiyo kuanzia mnamo 2016 hadi mnamo 2021.

Maisha ya awali na elimu

[hariri | hariri chanzo]

Mukhtar alizaliwa mnamo 23 Mei 1963 kwenye Eneo la Serikali ya Mitaa ya Manispaa ya Kano katika Jimbo la Kano huko Nigeria. Alipata masomo ya Shule ya Msingi ya Shahuchi na Shule ya Msingi ya Bweni ya Wasichana ya Shekara, na kisha Chuo cha Wasichana cha Serikali, Dala. Alihitimisha masomo yake na kupata shahada yake ya kwanza katika botania kutoka Chuo Kikuu cha Ahmadu Bello mnamo 1984. Baadaye alipata shahada yake ya pili na ya tatu kutoka Chuo Kikuu cha Bayero mnamo 1994 na 2005, mtawalia. Mnamo 2012, alijiunga na kozi ya bioteknolojia ya kilimo katika Chuo Kikuu cha Jimbo la Michigan . [1]

Mukhtar alianza kufanya kazi mnamo wa 1994 kwenye Chuo Kikuu cha Bayero Kano kwa nafasi ya mhadhiri msaidizi na akapanda cheo hadi kufikia kuwa profesa wa mimea mnamo wa 2010. Alibeba majukumu, kuanzia mratibu wa ngazi hadi mkuu wa Idara ya Sayansi ya Mimea.

Mukhtar ni mshirika wa Chuo Kikuu cha Northwest, Kano, na alikuwa kati ya wasimamizi wa kitaaluma ambayo ni waanzilishi. Alishika nafasi ya mkuu wa Kitivo cha Sayansi na kama naibu makamu mkuu wa chuo mnamo wa 2015, [2] na alifanikiwa kuongoza Kamati ya TEHAMA, Kamati ya Mfuko wa Hospitali, na Kamati ya Ufuatiliaji na Utendaji wa Bajeti.

Mukhtar alichaguliwa kwenye nafasi ya makamu wa pili wa mkuu wa Chuo Kikuu cha Shirikisho cha Dutse na Rais Muhammadu Buhari kwenye tarehe 14 Februari 2016. [3] [4] [5] [6]

Kwenye 30 Agosti 2023, Chuo Kikuu cha Azman kilimchagua Mukhtar kama makamu mkuu wa chuo kikuu. Kuchaguliwa kwake kuliweka, kwa sababu alikuwa mtu wa kwanza na mwanamke wa kwanza kuchukua nafasi ya juu zaidi ya uongozi wa chuo kikuu.

  1. ↑ admin. "Fatimah Batul Mukhtar" (PDF). Bayero University. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo Novemba 7, 2017. Iliwekwa mnamo Novemba 6, 2017.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. ↑ "Prof. Fatima Batul Mukhtar emerges 5th in the top 5 Nigerian Muslim Personalities of the Year 2019". Januari 15, 2020.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. ↑ Agencies (2019-11-11). "TETFUND scribe urges university lecturers to strengthen research development". TODAY (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2021-02-13.
  4. ↑ Nigeria, News Agency of (Januari 16, 2018). "TETFund launch projects worth N1.4bn at Jigawa university". TODAY.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  5. ↑ "Fatima Batul-Mukhtar -". NNN (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2021-02-13.
  6. ↑ Chila Andrew Aondofa (2019-11-22). "Prof Fatima Batul Mukhtar: 1st Female VC From North-West Nigeria". The Abusites (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2021-02-13.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]