Farrah Gray
Mandhari
Farrah Gray (Farrakhan Khalid Muhammad; [1] alizaliwa 9 Septemba 1984) ni mfanyabiashara, mwekezaji, mwandishi na mzungumzaji wa motisha kutoka Marekani.
Gray alilelewa upande wa Kusini mwa Chicago. Yeye ni mtoto wa kiongozi mweusi wa kizalendo marehemu Khalid Abdul Muhammad. Alianza kazi yake ya ujasiriamali akiwa na umri wa miaka sita akiuza losheni zilizotenenezwa nyumbani na mawe yaliyopakwa rangi kwa mkono nyumba kwa myumba. Na pia yeye ni Mkristo. [1]