Nenda kwa yaliyomo

Faraja

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Faraja, mchoro wa A. Kindler.

Faraja (kutoka neno la Kiarabu) ni msaada wa aina yoyote unaotolewa kwa mwingine aliyepatwa na dhiki, msiba au shida nyingine ili kumuinua kisaikolojia na kumfanya asijisikie mkiwa.

Katika michezo, mara nyingi aliyeshindwa anapata faraja akipongezwa na mshindi kwa jinsi alivyojitahidi[1].

Katika tiba, faraja ina nafasi muhimu pamoja na dawa[2].

Katika dini pia faraja ina nafasi muhimu kwa mtoaji na kwa mpokeaji vilevile [3].

Katika Uyahudi

[hariri | hariri chanzo]

Sehemu muhimu ya kazi ya manabii ilikuwa kuwafariji watu wa Israeli baada ya adhabu za Mungu kuwakatisha tamaa. Hivyo katika vitabu vyao tunakuta sura kadhaa zilizoitwa "Kitabu cha faraja", k.mf. Yeremia 30-31, lakini hasa Isaya 40-55.

Katika Ukristo

[hariri | hariri chanzo]

Injili inasimulia jinsi wanawake wa Yerusalemu waliojitahidi kumfariji Yesu akienda kusulubiwa (Lk 23:27) kama yeye alivyofariji wengi katika matatizo yao mbalimbali (Math 8:16-17; 11:28-30) [4]. Wakatoliki wanahimizwa kuendelea kumfariji kwa kufidia dharau anazopata bado katika dhambi za umati hasa za watu aliowapatia neema nyingi zaidi [5][6]

Mtume Paulo alisanisi habari njema katika maneno haya: "Na ahimidiwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, Baba wa rehema, Mungu wa faraja yote: atufarijiye katika dhiki zetu zote ili nasi tupate kuwafariji wale walio katika dhiki za namna zote, kwa faraja hizo, tunazofarijiwa na Mungu. Kwa kuwa kama vile mateso ya Kristo yanavyozidi kwetu, vivyo hivyo faraja yetu inazidi kwa njia ya Kristo" (2Kor 1:3-5)

  1. David Potter, The Victor's Crown: A History of Ancient Sport from Homer to Byzantium (2011), p. 28-29.
  2. Arthur W. Frank, The Renewal of Generosity: Illness, Medicine, and How to Live (2009), p. 2.
  3. David A. Leeming, Kathryn Madden, Stanton Marlan, Encyclopedia of Psychology and Religion (2010), p. 240.
  4. Ján Majerník, Joseph Ponessa, Laurie Watson Manhardt, The Synoptics: On the Gospels of Matthew, Mark, Luke (2005), p. 188.
  5. Papa Pius XI, Miserentissimus Redemptor, 8 May 1928
  6. Papa Fransisko, Dilexit nos, paragraph 152, published on 24 October 2024, accessed on 25 February 2025
Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Faraja kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.