Faraj Hawwar
Faraj Hawwar (Kiarabu: فرج الحوار; alizaliwa Hammam Sousse, 12 Februari 1954) ni mwandishi, mwandishi wa riwaya na mtafiti kutoka Tunisia.
Elimu
[hariri | hariri chanzo]Alikamilisha elimu yake ya msingi na sekondari katika Sousse, na mwaka 1978 alihitimu kutoka École Normale Supérieure, Tunisia, akisomea Lugha na Fasihi ya Kifaransa. Anaandika kwa Kiarabu na Kifaransa.[1][2]
Kazi
[hariri | hariri chanzo]Hawwar ni mwandishi wa riwaya wa Tunisia na mwanachama wa Umoja wa Waandishi wa Tunisia tangu mwaka 1993. Anaandika riwaya kwa Kiarabu na Kifaransa, na pia hadithi na mashairi kwa Kifaransa. Mwaka 1985, alichapisha riwaya yake ya kwanza Death, the Sea and the Rat (Kiarabu: Al-mawt wa-al-baḥr wa-al-ǧurad̲), na hadi sasa ameandika zaidi ya riwaya 16.[3][4][5]
Hawwar pia amechapisha vitabu kadhaa vya monografia, vikiwa ni pamoja na:
- Writers’ Metaphors and Rhetoricians' References (Kiarabu: Kināyāt al-udabāʼ wa-ishārāt al-bulaghāʼ),
- The Fragrant Meadows in Al Khatir’s Picnic (Kiarabu: al-Rawḍ al-ʻāṭir fī nuzʹhat al-khāṭir),
- Writing Desire (Kiarabu: kitābat al-raghbah) – utafiti juu ya kazi za Georges Bataille, kwa Kifaransa, 2013, na
- Dictionary of Tunisian Revolution (kwa Kifaransa, 2018).
Aidha, alitafsiri The Anthology of Tunisian Short Stories (2008) na Anthology of Tunisian Novels (2009) kutoka Kiarabu hadi Kifaransa, kwa kushirikiana na Hafez al-Hadidi.
Teses yake ya uzamivu (PhD) ilihusu swala la tamaa katika maandiko ya Georges Bataille, na pia amefanya tafiti kubwa juu ya masuala ya kijinsia katika urithi wa Kifaransa na Kiislamu cha Kiarabu.[6]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "فرج الحوار | جائزة كتارا للرواية العربية". 2020-07-14. Iliwekwa mnamo 2021-04-27.
- ↑ mominoun. "فرج الحوار: سبيل التسامح الإسلاميّ الخيار العلماني". Mominoun Without Borders (kwa Kiarabu). Iliwekwa mnamo 2021-04-27.
- ↑ Habib Salha (2008). Le roman maghrébin de langue française aujourd'hui: rupture et continuité. Faculté des lettres, des arts et des humanité de la Manouba. uk. 215. ISBN 978-9973-936-90-5. Iliwekwa mnamo 1 Mei 2021.
{{cite book}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Jean Fontaine (2009). Le roman tunisien a 100 ans, 1906-2006. Arabesques Edition. uk. 181. ISBN 978-9973-764-91-1. Iliwekwa mnamo 1 Mei 2021.
{{cite book}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "مقاربات في الرّواية والأقصوصة". البيان (kwa Kiarabu). Iliwekwa mnamo 2021-04-28.
- ↑ "الحوار، فرج ، 1954‒ Library of the Dominican Institute for Oriental Studies". alkindi.ideo-cairo.org. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-04-28. Iliwekwa mnamo 2021-04-28.
| Makala hii kuhusu mwandishi fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Faraj Hawwar kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |