Fanta

Fanta ni kinywaji cha soda kilichoanzishwa nchini Ujerumani mwaka 1941. Kampuni ya Coca-Cola imekuwa ikisambaza Fanta kote duniani tangu mwaka 1970. [2]
Aina
[hariri | hariri chanzo]Kuna zaidi ya ladha mia mbili za Fanta, zikiwemo ladha za chungwa, zabibu, nanasi, stroberi, tofaa, fyulisi, beri, tikiti maji, na limau. Ladha hizi hutofautiana kutokana na tamaduni mbalimbali na upatikanaji wa matunda hayo katika maeneo tofauti. [3]
Historia
[hariri | hariri chanzo]Fanta ilitengenezwa nchini Ujerumani mwaka 1940, wakati wa Vita vya Pili vya Dunia. Wakati huo, biashara kati ya Coca-Cola ya Marekani na tawi la Ujerumani ilisitishwa. Kwa kuwa Coca-Cola, haikuweza kusambaza syrup yake, Max Keith, kiongozi wa tawi la Ujerumani, alitengeneza kinywaji kipya kwa kutumia matunda yaliyosalia na jibini kiwandani. Mshirika wake alipendekeza jina “Fanta” kwa kinywaji hicho. [4]
Baada ya vita, biashara kati ya Marekani na Ujerumani ilirejea, na Fanta iliendelea kutengenezwa hadi mwaka 1949. Mwaka 1950, kampuni ya Società Napoletana Imbottigliamento Bevande Gassate,lirejesha Fanta ikiwa na ladha mpya ya machungwa. Coca-Cola ilinunua ladha hiyo mpya, ambayo inatumiwa hadi leo. [4]

Upatikanaji kimataifa
[hariri | hariri chanzo]Katika nchi nyingi, Fanta hutengenezwa kwa kutumia juisi ya machungwa, lakini nchini Marekani haitumii juisi hiyo. [6]
Nchini Meksiko, Fanta hutengenezwa kwa kutumia sukari halisi, wakati nchini Marekani hutumia syrup ya high-fructose corn.[7]
Nchini Uingereza, viwango vya sukari vilipunguzwa mwaka 2017 hadi gramu 4.6 kwa mililita 100 kutokana na ushuru mkubwa wa sukari. [8]
Katika nchi za Albania, Bosnia, Herzegovina, Croatia, Poland, Serbia, Romania, na Sweden, kuna ladha inayojulikana kama “Fanta Shokata.” Neno “Shokata” linamaanisha beri na msisimko kwa lugha ya Kiromania. Nchini Urusi,ladha hiyo inaitwa “Fanta Citrus",” na ni kama limau. Kinywaji hiki huwa na rangi nyeupe na huja kwenye chupa ya buluu. [9]
Mwezi Februari 2023, Coca-Cola ilitangazakuwa kinywaji cha “Lilt” (nanasi na zabibu) kilichokuwa kikisambazwa nchini Uingereza na Ireland, kitaanza kuitwa “Fanta Nanasi” na “Fanta Zabibu” kuanzia tarehe, 14 Februari 2023.
Fanta Afrika Mashariki
[hariri | hariri chanzo]Fanta ni maarufu sana Afrika Mashariki, hasa Fanta ya machungwa ambayo inawakilisha asilimia 80 ya mauzo ya Fanta katika eneo hili. Kuna ladha nyingine kama karakara, limau, na matunda twist pia. [10] Fanta ndiyo kinywaji cha soda maarufu zaidi nchini Kenya nakimeteuliwa kuwa soda inayopendwa zaidi.
Fanta hupatikana katika makopo ya alumini, chupa za plastiki, na chupa za kioo. [10]
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ https://www.fastcompany.com/90875506/exclusive-fantas-new-logo-ditches-the-fruit-just-like-its-soda
- ↑ https://by.coca-colahellenic.com/en/our-24-7-portfolio/sparkling/fanta#%3A~%3Atext%3DFanta%20was%20first%20produced%20in%2Cfor%20its%20bright%20refreshing%20taste
- ↑ https://the-soda.fandom.com/wiki/Fanta
- 1 2 https://www.heritagedaily.com/2024/08/the-haunting-history-of-fanta/153178
- ↑ https://logos.fandom.com/wiki/Fanta
- ↑ https://www.coca-cola.com/ca/en/brands/fanta
- ↑ https://www.beveragesdirect.com/products/mexican-fanta-orange?variant=42159396225181
- ↑ https://www.campaignlive.co.uk/article/fanta-changes-recipe-swerve-sugar-tax-part-biggest-shakeup-brands-history/1428378
- ↑ https://hr.coca-colahellenic.com/en/our-24-7-portfolio/brands-a-z/fanta/fanta-shokata
- 1 2 https://www.montyskenya.com/product-tag/fanta/