Fanny Clar
Clara Fanny Olivier (Februari 17, 1875 - Februari 24, 1944) alikuwa mwandishi wa habari na fasihi kutoka Ufaransa. Pia alijihusisha na siasa za kijamaa na harakati za ufeministi. Ingawa aliandika riwaya, mashairi na michezo ya kuigiza, alijulikana zaidi kwa hadithi za watoto.[1][2][3][4]
Maisha ya awali
[hariri | hariri chanzo]Clara Fanny Olivier alizaliwa Paris, Februari 17, 1875.
Maisha binafsi
[hariri | hariri chanzo]Clar alifunga ndoa na Emile Célié, na wakapata mtoto wa kiume aitwaye Jean (aliyezaliwa Februari 21, 1897). Baadaye aliishi na Raphaël Diligent (1884–1964) baada ya ndoa yake ya kwanza kuvunjika, aliyekuwa mchongaji sanamu na mchoraji, ambaye pia alichora baadhi ya vitabu vyake.
Fanny Clar alifariki dunia Februari 24, 1944.
Kazi
[hariri | hariri chanzo]Mnamo 1904, Fanny Clar alianza kuchapisha makala kwenye gazeti la anarchist Le Libertaire akitumia jina la “Francine,” ambako alikutana na Miguel Almereyda, baba yake Jean Vigo. Alijiunga na Ligi ya Kimataifa ya Elimu Bora ya Utotoni iliyoanzishwa na Francisco Ferrer mwaka 1908.Kuanzia 1912, Clar aliandika makala kwa wanawake katika gazeti lililopinga vita. Mwaka 1913, alishirikiana na Almereyda kwenye gazeti Le Bonnet rouge. Mwaka 1916, riwaya yake ilichapishwa kwenye gazeti la L’Humanité. Wakati wa Vita Kuu ya Kwanza, aliandika makala akishirikiana na mwanawe Jean Célié kwenye magazeti ya kijamaa. Pia alichangia kwenye gazeti la wanawake La Voix des femmes.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Vernet, Madeleine; Larivière, Éliane; Clar, Fanny; Hecquet, Marceline (1924). "Lettre ouverte aux gouvernements" [Open letter to governments]. La Mère Educatrice (kwa Kifaransa). 7: 81–82.
- ↑ "Echos". L'Humanité : journal socialiste quotidien (kwa Kifaransa). 13 Oktoba 1919. uk. 2. Iliwekwa mnamo 9 Januari 2023 – kutoka Gallica.
{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Louis Marchand (1920). "Preface, by Maurice Barrès". L'offensive morale des Allemands, en France, pendant la guerre: l'assaut de l'ame française (kwa Kifaransa). La Renaissance du livre. ku. v-. OCLC 1061208202.
- ↑ Clar, Fanny (1875-1944) (18 Novemba 2022). "BnF Catalogue général". Dictionnaire des anarchiste (kwa Kifaransa). Maitron/Editions de l'Atelier. Iliwekwa mnamo 9 Januari 2023.
{{cite web}}: CS1 maint: numeric names: authors list (link)
| Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Fanny Clar kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |