Familia (biolojia)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Pitio kulingana na tarehe 13:29, 11 Machi 2013 na Addbot (majadiliano | michango) (Bot: Migrating 87 interwiki links, now provided by Wikidata on d:q35409 (translate me))
Ngazi za uainishaji katika biolojia; ngazi ndogo za kati hazionyeshwi

Familia ni ngazi katika uainishaji wa kisayansi wa viumbehai. Familia ya wanyama au mimea hujumlisha spishi mbalimbali zilizo karibu.

Kwa mfano paka-kaya ni spishi mojawapo pamoja na spishi 41 nyingine ndani ya familia ya Felidae inayojumlisha paka pamoja na chui, simba, tiger n.k.

Ndani ya familia kuna jenasi mbalimbali (zinazojumlisha spishi za karibu zaidi); kila familia ni sehemu ya ngazi ya juu zaidi inayoitwa oda. Familia ya Felidae (wanyama wanaofana na paka) ni sehemu ya oda ya Carnivora au wanyama wala nyama.

Kwa kawaida majina ya kisayansi ya kila familia huishia kwa

- "idae" kama ni familia ya wanyama au - "aceae" kama ni failia ya mimea.


Familia kubwa sana zinaweza kugawiwa katika nusufamilia; vilevile oda kubwa sana inaweza kuwa na familia kubwa za kujumlisha ngazi ya familia.