Falsafa ya dini

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Alama za dini mbalimbali.

Falsafa ya dini ni utafiti wa kifalsafa kuhusu mada na mawazo makuu ya dini mbalimbali[1] na jinsi yanavyoathiri mwenendo wa watu binafsi na katika jamii.

Majadiliano kuhusu mambo hayo yalianza zamani na kujitokeza katika maandishi ya kwanza ya wanafalsafa wa Ugiriki wa Kale.

Utafiti huo unaenea kwa matawi mengine ya falsafa kama vile metafizikia, epistemolojia na maadili.[2]

Falsafa ya dini ni tofauti na falsafa ya kidini kwa kuwa inajadili masuala yanayohusu umbile la dini kwa jumla, si kuchunguza masuala yanayotokezwa na imani ya dini fulani. Hivyo inaweza kuchangiwa na watu wa dini yoyote na vilevile watu wasio na dini.[3]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. Taliaferro, Charles (1 Januari 2014). Zalta, Edward N. (mhr.). Philosophy of Religion (toleo la Winter 2014).{{cite book}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. Stanford Encyclopedia of Philosophy, "Philosophy of Religion."
  3. Evans, C. Stephen (1985). Philosophy of Religion: Thinking about Faith. InterVarsity Press. ku. 16–17. ISBN 978-0-87784-343-6. Philosophy of religion is not so much religious thinking as it is thinking about religion, a thinking which can be carried on by both religious and nonreligious persons.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mambo ya dini bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu mada hii kama historia yake au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.