Nenda kwa yaliyomo

Fainali ya Kombe la Dunia la 2014

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Fainali ya Kombe la Dunia ya mwaka 2014 lilifanyikia Maracana Rio de Janeiro, nchini Brazili[1]. Mechi hiyo ya fainali ilikuwa kama marudio ya fainali ya mwaka 1989 na 1990 ambazo zilikutanisha mataifa ya Ujerumani na Argentina.[2]

Taifa la Ujerumani ndilo liliibuka na ubingwa baada ya kuifunga timu ya taifa ya Argentina kwa bao 1-0, Bao hilo liliwekwa wavuni na mchezaji wa kijerumani Mario Götze na kuifanya Ujerumani kuibuka mabingwa kwenye mchezo huo[3].

Kufuatia ushindi huo Ujerumani walinyakua taji la nne la dunia. kupitia mchezo huo Kipa wa Ujerumani Manuel Nuer alitangazwa kuwa kipa bora wa kipindi hicho na akatuzwa tuzo ya kipa bora wa michuano[3]. Mchuano huo ulihudhuliwa na mashabiki wengi wa mpira duniani.[4]

  1. "Ujerumani ilivyoiduwaza Argentina fainali Kombe la Dunia 2014". Mwanaspoti (kwa Kiingereza). 2021-05-09. Iliwekwa mnamo 2025-10-14.
  2. "BRAZIL 2014: Ujerumani - Mabingwa wa Dunia!". Mwananchi (kwa Kiingereza). 2021-03-24. Iliwekwa mnamo 2025-10-14.
  3. 1 2 "Ujerumani ni bingwa wa kombe la dunia". BBC News Swahili. 2014-07-13. Iliwekwa mnamo 2025-10-14.
  4. "Ujerumani yanyakua Kombe la nne la Dunia – DW – 14.07.2014". dw.com. Iliwekwa mnamo 2025-10-14.