Fábinho (Tavares)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Fabinho akiichezea Liverpool mwaka 2018

Fábio Henrique Tavares (alizaliwa 23 Oktoba 1993, anajulikana kama Fabinho) ni mchezaji wa soka wa Brazil ambaye anacheza kama kiungo wa Liverpool F.C. na timu ya taifa ya Brazil.

Mchezaji hodari ambaye anacheza kama kiungo mkabaji, Fabinho pia anaweza kuwekwa ama kucheza kama beki wa kulia[1] au beki wa kati.[2] Fabinho mara nyingi anatazamwa kama mmoja wa viungo bora zaidi wa ulinzi duniani.[3][4]

Baada ya kuanza kucheza katika klabu ya Fluminense, alihamia Rio Ave mwaka 2012. Alitumia muda wake wote huko nje kwa mkopo, kwanza katika Real Madrid Castilla, na akacheza katika kikosi cha kwanza. Alitumia takribani miaka mitano akiwa AS Monaco, akicheza jumla ya michezo 233 na kufunga mabao 31, na walishinda ligi ya Ligue 1 mnamo 2016-17. Katika msimu wake wa kwanza akiwa Liverpool walishinda Ligi ya Mabingwa ya UEFA 2018-19. Ushindi wa Kombe la UEFA Super Cup 2019 ulifuatia na huku Fabinho akionyesha uwezo mkubwa uwanjani kupelekea Liverpool kushinda Ligi Kuu ya Uingereza 2019-20.

Fabinho alicheza mechi yake ya kwanza ya kimataifa akiwa na Brazil mwaka 2015, na alikuwa sehemu ya kikosi chao kwenye Copa América mnamo 2015, 2016 na 2021, na pia Kombe la Dunia la FIFA la 2022.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Shaw, Chris (30 January 2019). "Fabinho on Liverpool's right-back options v Leicester". Liverpool F.C. Iliwekwa mnamo 30 January 2019.  Check date values in: |date=, |accessdate= (help)
  2. Shaw, Chris (21 September 2020). "James Milner on Ajax victory, Fabinho at centre-back and more". Liverpool F.C. Iliwekwa mnamo 21 September 2020.  Check date values in: |date=, |accessdate= (help)
  3. Bate, Adam (November 2019). "Why Fabinho is now the Premier League's best holding midfielder". FourFourTwo. Iliwekwa mnamo 15 May 2021.  Check date values in: |date=, |accessdate= (help)
  4. "The 100 best male footballers in the world 2019", 20 December 2019. 
Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Fábinho (Tavares) kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.