Event:Wikimalkia 2025-26 campaign in Tanzania/Wikimalkia December 2025 Edit-a-thon in Tanzania
Karibu ujiunge na Wikimalkia 2025 Edit-a-thon in Tanzania, iliyoandaliwa na Jumuiya ya Wikimedia community kilimanjaro. Hili ni tukio la vitendo lenye lengo la kuwawezesha wanawake kushiriki kikamilifu katika shughuli za Wikipedia hapa Tanzania, pamoja na kuongeza na kuboresha maudhui yanayohusu wanawake katika Wikipedia ya Kiswahili.
Kupitia edit-a-thon hii, washiriki watapata fursa ya kujifunza na kushirikiana katika kuandika na kuhariri makala zinazohusiana na wanawake, utamaduni wa Kitanzania na Afrika, na maarifa ya jamii za ndani, huku wakichangia kukuza maarifa huria kwa wasomaji wa Kiswahili duniani kote.
Kwa nini Ushiriki?
[hariri | hariri chanzo]- Kuongeza uwakilishi wa wanawake katika Wikipedia ya Kiswahili.
- Kuimarisha maudhui kuhusu utamaduni na jamii za Kiafrika.
- Kujenga ujuzi wa wiki katika kutafsiri, kuandika, kufanya utafiti, na ushirikiano wa kidijitali.
Jiunge nasi, Changia, na saidia kukuza Wikipedia ya Kiswahili!
Ratiba
[hariri | hariri chanzo]Desemba 2025
Mahali
[hariri | hariri chanzo]Mtandaoni na ana kwa ana. (Maelezo ya eneo la ana kwa ana yatatangazwa hivi karibuni)